Saturday, November 29, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMSAIDIA FUNDI KUSHONA VIATU

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsaidia Fundi  viatu Abeid Yusuf Lukanga  ambaye ni mlemvu kushona viatu wakati alipofungu shina la wana CCM la Kiyunga mjini Mtwara akiwa katika ziara ya kikazi ya mkoani Mtwara kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa pamoja na wananchi, Katika ziara ape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga ripu katika jengo la ofisi ya kata ya Shangani mjini Mtwara.
 Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasneni Murji akizungumza na akina mama wajasiriamali Kata ya Rahaleo mjini Mtwara.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa kisima cha maji wa Chikongola.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha mmoja wa akina mama mara baada ya kuzindua kisima cha maji Chikongola.
 Baadhi ya akina mama wakihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa kwa kisima hicho.
 Ofisi ya CCM ya kata ya Chikongola iliyochomwa wakati wa vurugu za gesi mwaka jana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ukarabati wa ofisi ya CCM ya kata ya Chikongola iliyochomwa wakati wa vurugu za gesi mwaka jana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kata ya Jangwani kijiji cha Lwelu.
 Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasneni Murji akishiriki kucheza ngoma katika kijiji cha Lwelu.
Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasneni Murji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lwelu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni kwa waendesha bodaboda waliopata mafunzo kwa ufadhili wa mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiakikabidhi pikipiki kwa Ali Hasan mmoja wa waendesha bodaboda pikipiki hizo zimetolewa na Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiakikabidhi pikipiki kwa Said Chipangula mmoja wa waendesha bodaboda pikipiki hizo zimetolewa na Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji.
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiongozwa na waendesha pikipiki ukitokea mikindani.

 Waendesha Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akitoka Mikindani kuelekea Mtwara mjini.


No comments:

Post a Comment