
Maharusi Benson Mahenge na Godliver Joseph wakimeremeta mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika kanisa la Katoliki la Mtakatifu Augustino lililoko Mbezi kwa Msuguri Oktoba 29 na kufuatiwa na hafla ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya taifa Posta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita , FULLSHANGWE inawapongeza wanandoa hao na mungu awabariki na kuwajalia katika maisha yenu ya siku zote.

Mkurugenzi wa FULLSHANGWE John Bukuku kushoto akipozi kwa picha na na maharusi wakati alipokwenda kuwapongeza.

Wazazi wakiwapongeza maharusi wakati wa hafla yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta jijini Dar es salaam.

Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wanakamati waliofanikisha ndoa yao wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho Posta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment