TUTUMIE HABARI NA PICHA MDAU!!

MDAU UKIWA NA HABARI ZOZOTE ZA MICHEZO,BURUDANI,JAMII NA MITINDO USISITE KUTUTUMIA KWA EMAIL HII johnbukuku@gmail.com FULLSHANGWE NI YAKO.

Sunday, November 22, 2009

BUSTER RHYMES AFANYA KWELI FIESTA 2009, AMKUBALI CHID BENZ!

Buster Rhymes kulia akimfariji Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga aliyenyanyua mkono juu, kutokana na kuondokewa na baba yake mzazi Marehemu Mzee Alex Kusaga ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo mara baada ya kufanaya onyesho la kukata na shoka usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Posta Jijini Dar es salaam, Busta alifanikiwa kuziteka nyoyo za mashabiki kwa kiwango cha juu huku akisifu Tanzania na watu wake akisema ni watu wazuri wakarimu na akasema anafurhishwa sana na umati wa mashabiki uliokuwa umejitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta One Love 2009.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga alisema anamshukuru sana Buster Rhymes kwa kujali na kuwa na moyo wa huruma kwani onyesho hilo lilikuwa lifanyike Novemba 7 likaahirishwa kutokana na msiba huo hata hivyo Buster Rhymes alikubali kuja kufanya onyesho Novemba 21 pamoja na kazi zake nyingi akamshukuru sana na akasema onyesho hilo analitoa kama Dedication kwa Marehemu baba yake.
Buster Rhymes kulia akiwa na mkali mwingine aliyeongozana naye, huyu si mwingine ni Splifstar aliyeko kushoto wakiwadatisha mashabiki katika viwanja vya Posta Kijitonyama usiku wa kuamkia leo.
Mkali Buster Rhymes Jukwaani sasa! alistaajabu umati wa watu ulivyokuwa mkubwa na akasifu sana Tanzania na watu wake.
Hapa ndipo Buster Rhymes alipompa pongezi Chid Benz kabla hajapanda jukwaani kwa Swaga lililofunika Fiesta One love 2009 kwa wasanii wa bongo.
Mabaunsa walikukuwa na kazi ngumu baada ya uzalendo kuwashinda mashabiki na kutaka kuvamia jukwaa kutokana na hisia walizokuwa wakipata wakati Buster Rhymes anafanya mambo makubwa.
Msanii Pekee wa Tanzania Chid Benz aliyefanikiwa kuteka hisia za Buster Rhymes wakati akighani jukwaani, alifanya onyesho la kukata na shoka na alikuwa na nguvu za kucheza na kuimba wakati wote alipokuwa jukwaani, hongera Chid Benz.
Mashabiki kunyanyua juu mikono Hii haikuwa amri bali ilikuwa burudani tu.
Adam Mchomvu wa Clouds Radio kulia akiongoza burudani kwa mashabiki chini ya jukwaa.
Akudo Impact wao wakaonyesha shoo kivyao chini ya jukwaa, iilikuwa kali sana staili yao.
Huyu ndo yule mkali wa kurap anaitwa Cpwaa.
(HBC) Unawakumbuka hawa jamani mdau nao walikamua kikamilifu kuoka kulia ni Prof. J, Willy, na Terry enzi hizo wakijulikana kama kundi la Hardblasters.
Ikawa ni zamu ya Marlow kufanya vitu vyake.
Naye mzee wa mitulinga Profesor J. akakamua vilivyo katika jukwaa hilo la Fiesta One Love.
Vijana wa kazi THT wakiwajibika nadhani kwa sasa hawana mpizani jijini Dar es salaam.
Wakati wenzie wanaserebuka na Buster Rhymes yeye Farida hali ilikuwa mbaya sana maana alikuwa amebanwa kwenye kona ya vyuma hata muziki ulikuwa haupandi kabisa.

Witness akiwa amepagawa na mzee mzima Buster Rhymes ilikuwa si mchezo!

Chui wa Serengeti wafalme wa raha kamili wao ni rafiki wa kila mtu kama unavyoona wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti.
Kutoka kulia ni Sizzy Azizi wa B. Band, Bazo Komu wa TBC1, Nelly , Babla, Abuu meneja wa B. Band na Banana Zorro kiongozi wa B. Band nao walikuwepo kwenye tamasha la Fiesta One Love usiku wa kuamkia leo.
Meneja matukio na promosheni wa Serengeti Breweriers Bahati Singh katikati akionyesha One Love kwa Maunda Zorro kushoto na Baby Madaha.

Frolenso na Debora Nyangi wa Kalunde Band wakashow nao One Love ya Fiesta
Chui wa Serengeti wakawa rafiki wa Meneja uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda,
Gardiner G. Habash kama Kapteni wa Jahazi alikula kivazi hiki.
Baby Madaha katika pozi! unalionaje mdau.

Saturday, November 21, 2009

Mustafa Hassanali First Solo Art Exhibition to be Unveiled

Inspired by nature, the feel of the Morning Dew, The warmth of the Setting Sun, The chills of the Cool Weather,(a rarity in this Haven of Peace)…. It’s the Small things which bring Joy to Our Lives…
Mother Nature has given us in Abundance; it’s up to us how we use it as we go through this Journey called “Life”. Wastage is denying the Deprived of their Right by the Privileged Few…
“Hence Over the time since I Started My atelier we have been part of the Special Moments of So many People Lives and with each moment Came Left over Fabrics…. A pile which Kept on growing…”Hassanali Explained
The flamboyance and rich cocktail of Colour inspired this Collection of Art from Left over Fabrics and Haberdashery ranging from Khanga Kitenge, Bazein, and Satins. The Beauty of Mustafa Hassanali Signature mark to the world of Art shall bring a Different Voice that “WE CARE”
The Exhibition will run at Alliance Francaise From 23 to 28 November 2009 from 1000-1800HRS
Being Environment Conscious, Mustafa Hassanali has been selected as a Climate Change Icon by the British Council Tanzania for his role in creating an Initiative for a Better cleaner and Neater Future for Tanzanian through Art, Fashion, and Design.
Mustafa Hassanali’s commitment is to not only to promote the creative sector Industry especially Fashion in Tanzania , but also emphasise the Made in Tanzania Concept.
The Exhibition is part of Mustafa Hassanali Tenth Anniversary Celebration since His first Crowning Outfit Designed for Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu

NGUMI ZILIKUWA NZITO KUPITA KIASI BONDENI!!

Mabondia wa Tanzania Rashid Ally (kulia) na Anthon Mathias (kushoto) wakiwa na kocha wao George Sabuni katikati katika uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere mara baada ya kurejea kutoka nchini Afrika Kusini walikokuwa na mapambano ya ngumi na mabondia wa nchini humo, ambapo Wote walipigwa kwa KO katika Round ya 1 na ya 4 mapambano hayo yalifanyika katika jiji la Johanesburg, akizungumzia mapambano hayo bondia Rashid Ally amesema mabondia waliopigana nao walikuwa na nguvu za mikono kupita kiasi ndiyo maana walishushiwa kipigo mapema, ameongeza kwamba ili waweze kushinda mapambano yajayo wanahitaji mazoezi ya nguvu na ya muda mrefu sana kabla ya kupanda ulingoni.

HUKU NDIYO KUKUMBUKANA!!

Jamani baba kammiss mtoto, mtoto kammiss baba patamu hapo we angalia mwenyewe walivyokaa kwa utulivu wakisimuliana habari mbalimbali na kupeana zawadi wakati mama akishughulikia kutoa mizigo yake kweye uwanja wa ndege wa mawalimu J.K.Nyerere.

BUSTA RYMES ATUA JIJINI DAR, KUWASHIKA MASHABIKI KWENYE FIESTA LEO!!

Mwanamuziki Busta Rymes kutoka nchini Marekani (katikati) akitoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Mwalimu J.K.Nyerere mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kwa dege ya shirika la ndege la Emirates jioni hii, Busta amekuja kuwashika mashabiki wake nchini katika tamasha kubwa la Fiesta linalofanyika leo kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam ambapo pia wasanii mbalimbali watapanda jukwaani kuonyesha uwezo wao katika tamasha  hili ambalo ndiyo kubwa zaidi na hufanyika kila mwaka , wanamuziki wengi wa kimataifa kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakialikwa kuja kuonyesha kazi zao na kuburudisha mashabiki wao, Busta ni mmoja wa wanamuziki wanaoheshimika nchini Marekani kutokana na uwezo wake kimuziki
akiongozwa kuelekea kwenye Gari  huku akiwa amezungukwa na walinzi wake
Hapa akiingia kwenye Gari kuelekea Hotelini Movenpick huyu mwenye mwili mkubwa ni Mlinzi wake.

Gari lililomchukua mwanamuziki Busta Rymes likiondoka kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere  kuelekea Hoteli ya Movenpick jioni hii.

President of South Africa meets Miss World contestants!!

Yestarday the President of South Africa, Jacob Zuma, met this year's Miss World contestants at the Presidential Palace in Pretoria

MAMA SALMA KIKWETE ALIPOTEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA MAREKANI!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akimuonyesha albamu ya picha mbalimbali za kazi zinazofanywa na Taasisi ya WAMA Pernessa Seele ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya The Palm in Gilead ya nchini Marekani. Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo walimtembelea Mama Kikwete ofisini kwake jana kwa ajili ya kumshukuru katika jitihada zake za kupiga vita ugonjwa wa UKIMWI hapa nchini.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimuonyesha Pernessa Seele mkeka uliotengenezwa na wanawake wa Rufiji

Friday, November 20, 2009

RIPOTI YA ZOEZI LA UHAKIKI WA MADAI YA WALIMU HADHARANI!!

Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh akionyesha ripoti ya ukaguzi wa madai ya walimu wa Sekondari na vyuo.
Zoezi la Uhakiki wa madai ya waalimu na watumishi walio chini ya wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi lakamilika.
Akitolea ufafanuzi zoezi hilo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Ludovick Utouh amesema imegundulika kuwa katika idadi ya majalada 19,861 yaliyowasilishwa na yenye jumla ya Sh. bilioni 26.07 kati ya madai hayo yenye jumla ya shilingi bilioni 12.5 au asilimia 48 yamekubaliwa kwa malipo na madai ya shilingi bilioni 13.5 ambayo ni asilimia 52 yamekataliwa na kuonekana kuwa hayastahili kulipwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo nyaraka za kughushi.
Baada ya zoezi zima la ukaguzi wa madai hayo na kugundua kuwa kuna dosari au udanganyifu katika majalada hayo Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali imeishauri serikali ishughulikie tatio hilo la malimbikizo ya madai ya watumishi ili lisijirudie lakini pia serikali itoe fursa kwa walimu ya kukata rufaa kwa yeyote atakayedhani kuwa hakutendewa haki, pia mkaguzi huyo mkuu wa serikali na ofisi yake amependekeza kuwa walioghushi nyaraka wachukuliwe hatua za kinidhamu
Zoezi hilo lilianza mwezi Agosti 23. 2009 na kumalizika oktoba 31. 2009

Cafu’s special South African mission!

Marcos Evangelista de Moraes (Cafu).
Marcos Evangelista de Moraes – or Cafu as he is known by all in the football world - has won absolutely everything in a stellar player career.
He is Brazil’s most-capped player ever with 143 international appearances, has won the FIFA World Cup™ not once but twice, the UEFA Champions League with AC Milan, as well as the Italian Scudetto league title with Milan and AS Roma.
And after a highly decorated career he is continuing to use the power of football to reap even greater personal rewards.
One of six children born in Villa Irene - one of the poorest districts in Sao Paulo - the Brazilian legend established the Cafu Foundation after retiring from the game, raising funds to support education and sport programmes in the favelas of Brazil.
And Cafu was in Johannesburg today to meet South Africa’s 2010 FIFA World Cup™ Chief Executive, Dr Danny Jordaan, to discuss ways of supporting similar fundraising projects to help needy kids in South Africa
“South Africa and Brazil are very similar. We have the same social problems, same issues and same growing economies. And I am here in South Africa to avail myself to do whatever I can to assist South Africa’s World Cup efforts and to help to leave a legacy after the World Cup. I believe this World Cup is very special and that it will be the most successful in history. And I would like to assist in whatever way I can,” Cafu said after the meeting at Jordaan’s SAFA House office.
Cafu intends to canvass for financial support and establish a ‘We love Africa’ project in his name to support South African social projects and his first port of call was Jordaan’s office to brief him of his intentions.
Jordaan said many promising young South African footballers fell by the wayside, due to the vagaries of drug abuse and gangsterism, with Cafu saying this was also the case in Brazil and one of the main reasons he established his foundation.
“We’ve always said this World Cup is about more than 90 minutes of football. It must leave a social legacy. Like Brazil, we’re a developing country and the sport of the poor is football. I am delighted that a player like Cafu, one of the greatest players in world football and a wonderful role model, has come to talk about the social legacy of the World Cup and to lend his support in this area. We will definitely support his efforts and continue to engage with him on this matter,” said Jordaan, who added that Cafu would be attending the Final Draw of the 2010 FIFA World Cup in Cape Town on 4 December 2009.
While his first visit to South Africa is a short one, Cafu has been caught up in World Cup fever.
“I’ve played in many stadiums in the world and won many trophies. And the facilities here are very impressive, the stadiums, airports and hotels are among the best in the world. But I’ve been most impressed by the country’s people. Brazilian people and South African people are very similar in all respects. They are very warm and friendly. You feel the warmth of the people on the streets and see how much they want to host this World Cup. What I’ve seen here is amazing,” said Cafu.
While he thought the outside of the Soccer City stadium – that will host the opening match and final – was “unbelievable” with its distinctive calabash outer shell, Cafu was blown away when he got to see the inside of the 89 000-seater stadium.
“As a player seeing this magnificent stadium is very emotional,” Cafu said as he looked on to the pitch where Africa’s first World Cup will kick off 11 June 2010, adding “it gives me goose bumps”. www.fifa.com

Kilele cha Siku cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa ya Haki za Mtoto!!

Wawakilishi wa Baraza la Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Dkt Lucy Nkya, Mbunge wa Viti Maalum Iringa Mhe. Lediana Mungo'ngo' na wa Kwanza Kushoto ni Katibu Mkuu,Mariam Mwaffisi mara baada ya kikao kati ya wawakilishi hao wa Watoto na Mhe.Naibu Waziri. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kupata majibu ya maswali mbalimbali kutoka kwa Waziri kuhusu masuala ya Watoto katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa Kuhusu Haki za Mtoto (CRC).
Picha na (Asteria V. Muhozya wa Jinsia Wanawake na Watoto)

Taarifa ya msiba mbeya!

Dada Alice J.B. Kibopile (Alice Ngubwene) anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi mpendwa,John Burton Kibopile wa Forest Mbeya,kilichotokea jana tar 19/11/2009 asubuhi katika hospitali ya rufaa Mbeya,Marehemu Jonh ampaka anafariki alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa w shinikizo la damu na kisukari.Aidha mazishi yamepangwa kufanyika nyumbani kwake Forest,Mbeya siku ya jumamosi (kesho) tarehe 21/11/2009.Kwa taarifa zaidi wasiliana na Paul 0754294999,Patrick 0784255413,Alice 07i6501676/0733606

YANGA YATEMA WACHEZAJI WATANO, MMOJA KATI YAO AHAMISHWA KWA MKOPO!!

Boniface Ambani mmoja wa wachezaji waliotemwa na Yanga.

Uongozi wa timu ya Yanga leo umetangaza kuwatema rasmi wachezaji wake watatu, wawili kuwahamisha kwa mkopo na mmoja ambaye mkataba wake umekwisha katika klabu hiyo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani Afisa habari wa klabu hiyo Louis Sendeu amesema wachzaji walioachwa ni Khamis Yusuf, Mkenya james Shikokoti na mkenya mwingine Boniface Ambani.
Lous Sendeu ameongeza kuwa mchezaji Vicent Barnabas amehamishwa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Africa Lione iliyoko chini ya Mbunge wa Singida Mjini Mohamed Dewji maarufu kama (Mo), kwa upande wa mchezaji Mike Baraza ambaye ni raia wa kenya Msemaji huyo wa Yanga amesema mchezaji huyo mkataba wake ulikwishamalizika katika timu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi kuu ya Vodacom japokuwa imekuwa ikisuasua katika mwenendo wa ligi kuu ya mwaka huu 2009 ambapo timu ya Simba inashika usukani kwa kujikusanyia pointi zote 33 katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ikiwa imeshinda michezo zake zote
Mchezaji Mike Baraza katika siku za hivi karibuni ameripotiwa kwenda katika klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam na hata yeye mwenyewe hajakataa wala kukubali kama kweli ameshasaini kuichezea timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Kitu muhimu ni kusubiri wakati uongozi wa Simba utakapotangaza mchezaji gani mpya ataingia katika timu hiyo na mchezaji gani atahamishwa kwa mkopo kwani kocha mkuu wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri amesema hayuko tayari kuacha mchezaji yeyote katika timu hiyo kwani karibu wote wana kiwango kizuri labda wanaweza kuhamishwa kwa mkopo tu kwenda kwenye klabu nyingine na kuongeza wachezaji wapya ili kuongeza nguvu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa ya kombe la washindi.

Mpango mkakati wa usafi wa jiji la Dar waanza!.

Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Temeke Ally Hatibu akitoa ufafanuzi kwa Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi. Magreth Kinabo (katikati)kuhusu mpango mkakati wa miaka mitatu ya usafi wa mazingira katika manispaa hiyo wenye lengo la kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali. Kulia ni Bw. Jumanne Muhogo na Ernest Mamuya maafisa Afya wa manispaa hiyo.
Wafanyabiashara katika soko la Buguruni ,manispaa ya Ilala wakiendelea kuuza biashara mbalimbali vikiwemo vyakula katika mazingira machafu hali ambayo ni hatari kwa afya za watumiaji.


Centurion Casillas tells Real to focus!

Iker Casillas
Fresh from winning his 100th Spain cap, goalkeeper Iker Casillas returns to club duty with Real Madrid insisting they mustn't start thinking about the 'Clasico' against Barcelona in ten days' time.
Real sit a point behind champions Barcelona going into Saturday's home match against Racing Santander and Casillas believes Real can't start getting ahead of themselves.
"The president (Florentino Perez) has made a great effort for this season and we have to keep looking forward, not to the Champions League final at the Bernabeu (Real's home ground) or the game against Barcelona, but the next game against Racing Santander," said Casillas, who reached the 100-cap mark in last weekend's friendly against Argentina.
Despite heavy summer investment, Real won't be matching Barcelona's treble of last season after they were knocked out of the King's Cup by third-division Alcorcon in new coach Manuel Pellegrini's first major setback.
Pellegrini has had a public row with 33-year-old veteran Guti - who could be on his way out of the club after 14 years of service - but insists he has a good rapport with his players. "It is a great group and I have a good relationship with the players. I know what I am doing," said the Chilean coach.
Racing hope the appointment of new coach Miguel Angel Portugal can lift the players for the Real trip after the club parted company with Juan Carlos Mandia. Cristiano Ronaldo has said he is ready to return against Racing following an ankle injury but Pellegrini is likely to choose to give the Portuguese star more time with the game at Barcelona on the horizon story

La Palmier:Christmas Crakers !


Thursday, November 19, 2009

RAIS JAKAYA AWALAANI TFF KWA KUWAFUNGIA WACHEZAJI MIEZI SITA!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amelinyanyua juu kombe la FIFA la dunia wakati alipozindua rasmi ziara ya kombe hilo hapa nchini na kupiga nalo picha jioni hii kwenye uwanja wa taifa rais aliingia kwenye kibada maalum kilichojengwa kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuhifadhia kombe hilo akalibeba na kulinyanyua juu huku akilibusu kombe hilo , Rais Jakaya amemtaka rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Rodger Tenga pamoja na kamati zake kufanya kazi ya kusimamia na kuinua kiwango na vipaji vya mpira wa miguu nchini badala ya kusimamia timu ya taifa tu na mapato ya milangoni kwani hawako TFF kwa ajili ya kujenga nyumba zao Binafsi bali wapo kwa ajili ya kuendeleza na kukuza soka nchini, Rais Jakaya amelaani kitendo cha shirikisho hilo kuwapa adhabu ya kuwafungia muda mrefu hadi miezi sita wachezaji na kusema hiyo ni kuwakomoa na kudidimiza vipaji vyao badala ya kuviendeleza ziara ya kombe la FIFA la dunia inaratibiwa na wadhamini wa kombe hilo Cocacola na linatembezwa nchi mbalimbali Duniani, aliyeko kulia katika picha ni Hedi Hamer mwakilishi wa FIFA.
Wasanii maarufu Afrika mashariki walikuwepo pia ilikuleta burudani mbalimbali wakati wa mapokezi ya kombe hilo kama unavyowaona kuanzia kulia ni AY, Nameless kutoka Kenya na Chid Benzwakiwa wamepozi kwenye picha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwasili kwenye uwanja wa taifa jioni hii ili kuzindua rasmi ziara ya kombe hilo nchini kushoto ni mke wake Mama Salma Kikwete na kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera wakiiwa wameongozana na rais.
Washereheshaji Babra Hassan na Gerald Hando wa Radio Clouds waliosimama kulia wakisikiliza maagizo ya waratibu wa ziara hiyo Cocacola.
Walikuwepo warembo pia kamaunavyoona mwenyewe.
Kikundi cha halaiki kikitoa burudani kwenye uwanja wa taifa mara baada ya kombe hilo kuwasili kwenye uwanja huo.

Huu ni msafara wa pikipiki uliokuwepo ili kusherehesha mapokezi ya kombe hilo.
Ndege iliyobeba kombe hilo ikiwasili kwenye uwanja wa mwalimu J.K. Nyerere.
Kikundi cha Simba Thietre kikitumbuiza kwenye uwanja wa ndege wa mwalimiu J.K.Nyerere leo jioni wakati wa mapokezi ya kombe la FIFA la dunia lililowasili leo nchini.

MTANGAZAJI RADIO TIMES AJITOSA UCHAGUZI MPIRA WA KIKAPU!

Selemani Semunyu akirudisha fomu ya kuwania nafasi ya kamishna katika kamisheni ya watoto katika shirikisho la mpira wa kikapu TBF

Mjue Mwandishi wa habari pekee na Mtangazaji wa radio Times Selemani Semunyu aliyejitokeza kuwania nafasi ya kamisheni ya Watoto katika Shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF
jamaa ni mdau wa mpira huo na mchezaji aliyewahi kucheza kikapu katika timu ya Bees ya Tabora,timu ya Shule ya Sekondari ya Uyui, Young Worrios ya Morogoro na Shule ya Sekondari Kigurunyembe ya mkoani humo.
hamasa katika kikapu kuendeleza watoto na kuibua vipaji ndio mtazamo na malengo yake ni wakati sasa wa kuchagua viongozi wa ukweli watakao leta tija katika kikapu hasa damu mpya

ALGERIA YAFUNGA MDOMO WA MISRI, YAKATA TIKETI YA AFRIKA KUSINI 2010!

Kikosi cha Algeria.
Goli la Algeria lililopatikana kipindi cha kwanza Dakika ya 40 limewapa ushindi wa kihistoria Algeria dhidi ya Misri usiku wa kuamkia leo katika mechi ya (play off) iliyochezwa nchini Sudan.Kwa ujumla mchezo ulikuwa ni mkali na wenye kasi sana...wallahi waarabu wana fitina sana,
Rafu na ubabe vilitawala mechi hii na kila upande wakijaribu kucheza kwa makini kuepuka kupoteza mchezo, hata hivyo algeria ndiyo wamekuwa vinara wa mchezo huo baada ya kukata rasmi tiketi ya kwenda Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la dunia mwaka ujao 2010.
Mchezo huo ulikuwa wa marudio baada ya mshindi kutopatikana katika mchezo wa awali ulichezwa nchini Misri,
Kukiwa na ulinzi mkali kutokana na hofu iliyokuwa imetanda juu ya uwezekano wa mashabiki wa timu hizo mbili kushambuliana kutokana na uhasama wa miaka mingi, Shirikisho la mpira Afrika CAF liligawa tiketi zipatazo elfu 9000 kwa mashabiki wa soka kutoka Misri na Algeria na walikuwa wametenganishwa katika maeneo ya kukaa wakati wa mchezo huo ili kusitokee vurumai yoyote kama zilizotokea Katika mchezo wa awali nchini Misri ambapo mashabiki wapatao 30 hivi walijeruhiwa.

Wednesday, November 18, 2009

Big Brother Revolution: Images from Day 72!

Day 72 on M-Net’s Big Brother Revolution and ‘The Industrial Revolution’ is in full flow as the remaining housemates test some of the world’s oldest and greatest mysteries. The housemates have been given a number of scientific myths that they are to test and must all work together. The myths to be tested include: Can you make good luck? Who has the highest pain threshold – men or women? Gravity – can it be overcome? Watch this week’s task in progress by tuning in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199. For more information, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother

Redknapp fears for managers' future!

Harry Redknapp.
Harry Redknapp has spoken out on his fears for the future of homegrown managers within the English game.
The current Tottenham Hotspur boss began his career with ten years in the lower divisions at Bournemouth but insists that the 'learn your trade' route has been closed to the managers of the future.
"Six or seven bad results and you're coming under pressure. The younger managers don't get the opportunity, as soon as you have a bad spell you're out of work," said Redknapp.

There are lads in the lower divisions here who have got great talent but probably won't get an opportunity
Harry Redknapp on up-and-coming English managers
"Ten years at Bournemouth was great grounding for me. There are lads in the lower divisions here who have got great talent but probably won't get that opportunity because they are not fashionable names.
"These owners would rather bring some fashionable name from abroad, Spain or Italy, and give them a chance. It will hinder the chances of the lads in this country. There's nothing like learning your trade lower down."
Redknapp was speaking at the inaugural dinner of the League Managers' Association Hall of Fame 1000 club, celebrating the 18 men to have managed more than 1,000 domestic league or cup matches.
Redknapp has clocked up 1,134 matches at Bournemouth, West Ham, Portsmouth (twice), Southampton and Tottenham.

FIESTA ONE LOVE NI KUSHOO LOVE TU!!

Watangaji wa Redio Clouds Zamaradi Mketema kushoto na Ephraim Kibonde katikati wakishoo love na Meneja uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda wakati walipokuwa wakiongea moja kwa moja na watangazaji waliopo Studio kuu Mikocheni maarufu kama (Mjengoni) leo asubuhi kuzungumznia maandalizi ya tamasha kubwa la Fiesta litakalofanyika Novemba 21 katika viwanja vya Posta Kijitonyama, kulia ni meneja matukio wa kampuni hiyo Bahati Singh.

SERENGETI YADHAMINI KISURA WA TANZANIA KWA MILIONI 35!!

Meneja Uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda kulia akikabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi Milioni 35 kwa meneja mradi wa Kisura wa Tanzania Grace Kilembe huku kisura wa Tanzania 2008 Emmy Nelau na Meneja mkuu wa Serengeti Winston Kagusa waliosimama katikati wakishuhudia tukio hilo lililofanyika kiwandani hapo, aliyesimama kushoto ni Brand Manager wa Kampuni hiyo Nandi Mwiyombela, shindano la kisura wa Tanzania linatarajiwa kufanyika Disemba mosi mwaka huu kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar se salaam.

KOMBE LA DUNIA KUWASILI KESHO NCHINI!!

Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Taifa juu ya maandalizi ya ujio wa kombe la Dunia linalotarajiwa kuwasili kesho na kuzinduliwa kesho hiyohiyo na Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete saa kumi jioni, ambapo pia mashabiki mbalimbali watapata fursa ya kupiga nalo picha kwa kumbukumbu kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika nchi nyingine.

MITSUBISH PAJERO YA FIESTA (ONE LOVE) HADHARANI!!

Meneja Uhusiano wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akiweka saini kwenye gari aina ya Mitsubishi pajero linalotarajiwa kutolewa kwa mshindi wa bahati nasibu mashabiki wa Fiesta One Love itakayofanyika sambamba na tamasha hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya posta Kijitonyama, mashabiki watapata nafasi ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo kutokana na tiketi zao walizokata ili kuingia kwenye tamasha hilo ambapo wasanii mbalimbali watatoa burudani kutoka hapa nchini na nje ya nchi akiwemo mkali wa Hiphop kutoka nchini Marekani
Busta Rymes, kweli hii ni Fiesta one Love mdau.
Meneja Matukio na Promosheni wa Serengeti Breweriers Bahati Singh naye alipata nafasi ya kuweka saini katika gari hilo.
Mwandishi wa habari Kambi Mbwana kutoka New Habari Cooparation 2006 akiongoza waandishi wenzake wakati wa kuweka saini zao kwenye gari dogo aina ya Mitsubish pajero litakaloshindaniwa na namshabiki wa Fiesta One Love katika bahati nasibu itakayofanyika wakati wa Tamasha hilo kubwa nchini litakalofanyika jumamosi kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama.

Zamzibar Sauti za Busara Festival (Artist) 2010!

Juliana Kanyomozi from Uganda.
Juliana Kanyomozi is reigning Artiste of the Year (2008-09) in Uganda and one of the country’s favourite pop musicians. She started singing during infancy and began a professional career in music in the mid-1990s. Among her many hits include: Say It, Mama Mbire, Taata Wa Baana, Nabikoowa, Kibaluma, Usiende Mbali and the pivotal rendition of Philly Lutaaya’s Diana.
In Juliana’s quest to achieve her musical dreams, she teamed up with Uganda’s biggest music producer Steve Jean, who wrote and produced her first solo single, ‘Say It’. The single soared to the top of every national music chart and was a hit in all Uganda’s night clubs and entertainment spots. By the time her second single ‘Seven Days’ was released, Juliana was a sought after artist for concerts and events around Uganda including curtain raising for big names like Youssou N’dour. Her first local language [Luganda] duet, ‘Taata wa Abaana’ with Bobbi Wine was another number one hit that further catapulted Juliana, being the most played song on Ugandan radio in 2004. Another collaboration with Bobbi Wine, ‘Mama Mbire’, was a tribute to Ugandan mothers. For her debut album, Juliana again teamed up with Steve Jean and together, they produced Nabikoowa, the title track being another hit single. ‘Nabikoowa’ tells the story of a mistreated woman in a relationship who decided that enough damage had been done and rose up to tell the man so. Of course, this struck a chord with many women and and even male fans in Uganda. At the 2005 PAM Awards, Juliana swept the event winning four prizes including Female Artist of the Year, Song of the Year, Best R&B Single and Best R&B Artist.
An estimated six million people have seen Juliana perform on stage in Uganda. In addition, she has performed in UK, Sweden, Holland, UAE, USA, Nigeria, South Africa, Rwanda and Burundi.
Juliana’s second album, Kanyimbe (Let Me Sing) was released in 2007, verifying her talent. It is currently the biggest selling album in Uganda’s music stores. Including hits like Usiende Mbali, Mundeke, Diana and Sirina Mulala, the album is played daily on all the local FM stations.
Juliana is actively involved in works of charity within Uganda, and a silent Patron of IAM Children’s Orphanage in Kampala. She is actively involved in activities that discover and nurture talent in Uganda, a vigilant artist on issues of copyright law and mother to a son of six years.

MAMA KIKWETE NA MATUKIO YA ZIARA YAKE MKOANI SINGIDA!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amebeba kibuyu mara baada ya kukabidhiwa na wanawake wa kabila la wataturu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika mkoa wa Singida. Mama Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.(Picha na Juma Kengele - Ikulu)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelekezo kutoka kwa Mikasi Mpembee kuhusu jinsi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ya uyanjo VICOBA inavyofanya kazi. Taasisi ya WAMA iliichangia Uyanjo VICOBA Tshs.1,000,000/= fedha ambazo zitatumika kuinua mtaji wa biashara.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwakabidhi wanafunzi wa shule ya sekondari Itigi msaada wa magodoro 20 kwa ajili ya hosteli ya wanafunzi wasichana wa shule hiyo.

Wanafunzi walemavu wa shule ya msingi Kizega wafanya vizuri katika mitihani yao ya darasa la saba!!

Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi mkoani Singida
Na Anna Nkinda - Maelezo, Iramba
18/11/2009 Wanafunzi wenye ulemavu wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa baada ya wazazi wao kuona umuhimu wa kuwapeleka shule kwa wakati jambo ambalo limeifanya Serikali kuwapatiwa huduma mbalimbali wanazostahili kutokana na mahitaji yao.
Hayo yamesemwa jana na Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kizega yenye kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu Isaack Dagharo wakati mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kujionea maendeleo ya elimu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika wilaya ya Iramba.
Mwalimu Dagharo alisema kuwa shule hiyo ina makundi matatu ya aina tatu za walemavu ambao ni walemavu wa macho (wasioona) 15, walemavu wa ngozi (albino) 18 na walemavu wa viungo wawili hivyo kuifanya idadi ya wanafunzi kuwa 35 kati ya hao wavulana ni 25 na wasichana ni 10.
Aliendelea kusema kuwa wanafunzi wote 10 walemavu waliofanya mitihani ya darasa la saba tangu mwaka 2006 hadi mwaka 2008 waliweza kufaulu mitihani yao na kujiunga katika shule za Sekondari Mpwapwa, Shinyanga, Kinambeu na shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora .
"Kutokana na kutokuwa na shule maalum ya walemavu katika mkoa wa Singida wanafunzi hawa wanasoma na wanafunzi wasio walemavu kwa kuchanganyika madarasani lakini wanafunzi walemavu wao wanaishi katika baweni yaliyopo hapa shuleni", alisema Mwalimu Dagharo.
Shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia hasa vitabu vya Braille kwa wasioona hii imesababishwa na mabadiliko ya mitaala ya mara kwa mara, kukosekana kwa maji safi na umeme, upungufu wa thamani katika bwalo la chakula hasa meza na viti.
Alisema, "Changamoto zingine ni kukosekana kwa usafiri wa gari, kukosekana kwa lotion maalum, kofia na miwani kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili ya kujikinga na jua pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo".
Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleao (WAMA) aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao kwa kufanya hivyo matokeo yake watayaona hapo baadaye.
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1959 ikiwa ni shule ya wanafunzi wa kawaida lakini mwaka 1992 kitengo cha wanafunzi walemavu wasioona kilianzishwa kwa kuwaandikisha wanafunzi wanne tangu kuanzishwa kwake hadi sasa kitengo hicho kinawezeshwa na Halmashauri ya wilaya ya Iramba na wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi.
Taasisi ya WAMA pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu waliichangia shule hiyo zaidi ya shilingi milioni tatu na laki tano ili ziweze kuwasaidia kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi hao pia waliwapatia mafuta ya kupikia, mafuta ya taa, unga wa ngano, mchele, mahindi, maharage, sukari pamoja na chumvi.

Big Brother Revolution: Images from Day 64 - SUNDAY NOVEMBER 15!

Day 64 on M-Net’s Big Brother Revolution and the housemates prepare for this week’s nerve-wracking eviction news. When the announcement came it was time for Mozambique’s capeiro-loving Leonel to say goodbye to the series and to the massive USD 200 000 winner prize as he was voted out of the show having gotten the least votes from audiences. Tune in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199 and for more information, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Last nights’ show also featured performances from Botswana’s Cybil Nite and Kenya’s Collo.

Tuesday, November 17, 2009

MSEKWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO (NCAA)

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige kulia akiongea na wanahabari katika makao makuu ya Wizara hiyo leo wakati alipozungumziamabadiliko ya tarehe ya upandaji miti ambayo ilikuwa ikifanyika kila mwaka Januari mosi na kuwa Aprili mosi kutokana na mabadiliko ya waraka wa Waziri mkuu na. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kubadili siku ya kupanda miti kutoka January Mosi na kuwa Aprili Mosi kila mwaka rasmi kuanzia mwaka kesho.
Wakati huohuo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dr.Ladslaus Komba imesema Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano Mh. Pius Msekwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro (NCAA)
Na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Shamsa Mwangunga amewateuwa wajumbe wa bodi ya Mamlaka hiyo ambao watasaidiana na mzee Msekwa ni Mh. Job Y. Ndugai Mbunge wa Kongwa, Bw. Metui Ole Shaudo- Mwenyekiti Baraza la Wafugaji ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na kilimoTanzania, Mh. Lucas Selelii -Mbunge Nzega, Mh. Halima Mamuya -Mbunge Viti maalum Arusha na Bw. Emmanuel Lomayani -Mwakilishi wa wafanyabiahara wa mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Bw. Donatius Kamamba- mkurugenzi idara ya mambo ya kale Wizara ya Maliasili na utalii, Bw. Deogrtias Ntukamazina- Katibu mkuu Mstaafu Utumishi, Bw. Yona Nko wa ArushaBw. George Kaindoh - Mshauri Mwelekezi, Mjumbe kutoka Jeshi la Polisi na Bw. Bernard Murunya - Mhifadhi mkuu hifadhi ya Ngorongoro kuwa Katibu wa bodi hiyo katika picha kushoto kwa Naibu Waziri ni Felician Kilahama Kaimu Katibu Mkuu na mkurugenzi wa misitu na nyuki.

Baptista agent plays down Spurs link

Julio Baptista
The agent of Julio Baptista has brushed aside reports linking his client with a move to Tottenham Hotspur in the winter transfer window.
According to reports in Italy, Roma are keen on Spurs' wantaway striker Roman Pavlyuchenko and are ready to offer the Brazilian in return for the Russian.
But Herminio Menendez said: "There is no truth in these reports claiming he is set for an exchange in January.
"Julio is currently away with the national side. Any possible discussion is postponed until the future."
The former Arsenal player has been linked with a move away from the Stadio Olimpico since the summer. Baptista scored nine goals in 27 league appearances for I Giallorossi last season.
However, he has struggled in his second campaign in Rome and has yet to find the back of the net in five Serie A appearances. The 28-year-old is under contract with Roma until June 2012. By http://www.fifa.com/

President Kikwete meets Ban ki- Moon in Rome!

President Jakaya Mrisho Kikwete meets the UN Secretary General Ban-ki-Moon at the FAO Headquarters in Rome during the World Summit on Food Security yesterday.
President Jakaya Mrisho Kikwete in discussion with the Minister for Agriculture Stephen Wassira and Zanzibar's Minister for Agriculture,Natural Resources,environment and Cooperatives Mr.Burhani Saadat Haji at the FAO Headquarters during the plennary session of the World Summit on Food Security held in Rome yesterday(photos by Freddy Maro).



President Kikwete meets FAO Director General Mr. Jacques Diouf in Rome

The FAO Director General Mr.Jacques Diouf escorts President Jakaya Kikwete out of his Rome office shortly after they held talks at the FAO headquarters this morning.President Kikwete is in Rome to attend the World Summit on Food Security(Photos by Freddy Maro)

President Kikwete address World Summit on Food Security in Rome!!

President Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech duringtheWorld Summit on Food Security at FAO Hedqarters in Rome yesterday(photo by
Freddy Maro)


MAMA TUNU PINDA ZIARANI MKOA WA LINDI

Mke wa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akimkagua macho mtoto Nasra Muhidin wa Kituo cha yatima na waathirika wa ugonjwa wa ukimwi cha UWAVITA cha Liwale wakati alipokitembelea akiwa katika ziara ya Waziri Mkuu mkoani Lindi.

Wilaya ya Manyoni yajenga wodi ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano

Mama Salma kikwete akiwa amevaa vazi la kiasili la mkoa wa Dodoma
Na Anna Nkinda - Maelezo, Manyoni
17/11/2009 Jumla ya Tshs. 84,807,922/= zimetumika katika ujenzi wa wodi ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni iliyopo mkoani Singida.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Fotunata Malya wakati alisoma taarifa ya ujenzi wa wodi hiyo kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo.
Malya alisema kuwa ujenzi wa wodi hiyo ambao ulianza mwezi wa tisa mwaka 2007 na kukamilika mwezi wa tano mwaka huu umegharamiwa na Serikali kuu ambayo imetoa Tshs. 82,579,000/= pamoja na Halmashauri ya wilaya ambayo imetoa Tshs.2,228,300/=.
Alisema, "Ujenzi wa wodi hii ni matokeo ya kuongezeka kwa mahitaji ya mahali pa kulaza watoto kutokana na kuwepo kwa wodi ndogo isiyokuwa na nafasi ya kutosha. Msongamano huo ulifikia kiasi cha wagonjwa wawili au zaidi kulazwa katika kitanda kimoja".
Mkurugenzi huyo alisema kwamba wodi hiyo inakabiliwa na upungufu wa vitanda 40, magodoro 40, mashuka 240, vyandarua 80, mablanketi 80, makabati madogo ya ukutani 40, Oxygen Concentrator machine mbili, ENT set 10, Fumes/dust sucking machine moja na Resuscitation kit nne. Alizitaja gharama ya vifaa hivyo kuwa ni Tshs.25,678,000/=.
Akiongea na wananchi wa wilaya hiyo mara baada ya kufungua wodi hiyo Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa kujengwa kwa wodi hiyo kutaboresha huduma ya tiba kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na hivyo kupunguza vifo vyao.
Ili kupunguza tatizo la vifo vya kina mama wajawazito na watoto Taasisi ya WAMA iliipatia Hospitali hiyo msaada wa vitanda vya kujifungulia viwili, Delivery kit moja, vitanda vya Hospitali vinne, magodoro manne,mashuka nane,chombo cha kusikilizia mapafu au mapigo ya moyo (Stethosope) moja na mashine ya kupimia ugonjwa wa moyo moja. Thamani ya vifaa vyote ni Tshs.3,239,800/=.
Wilaya ya Manyoni ina hospitali tatu moja ni ya serikali na mbili ni za mashirika ya dini ambazo ni St. Gaspar Itigi na Kilimatinde, vituo vya afya vinne vitatu vya serikali na kimoja ni cha shirika la dini na zahanati 48 kati ya hizo 38 ni za serikali na kumi ni za mashirika ya dini na watu binafsi.

TAARIFA YA MSIBA WA MZEE ABUSHIRI KILUNGO!

MZEE ABUSHIRI KILUNGO (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO (16/11/2009) NYUMBANI KWAKE TANDIKA,MTAA WA KIVUNGO BAADA YA KUUGUA UGONJWA WA KISUKARI KWA MUDA MREFU.
MAREHEMU KILUNGO AMBAYE ALIWAHI KUWA NAIBU MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM MIAKA YA NYUMA NA PIA ALIWAHI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA DAR (DRFA).
MAREHEMU KILUNGO AMEACHA MKE NA WATOTO WATANO WATATU WAKIWA NI WA KIUME NA WAWILI WA KIKE.MAZISHI YATAFANYIKA LEO (17/11/2009) SHAMBANI KWAKE TUANGOMA,NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR ES SALAAM.
TUNAMUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MZEE WETU ABUSHIRI KILUNGO MAHALI PEMA PEPONI
-AMIN

Monday, November 16, 2009

Uhasama wa Algeria na Misri wazidi

Timu ya Taifa ya Misri
Timu ya Taifa ya Algeria.
Vikosi vya usalama vimepelekwa kuulinda ubalozi wa Misri mjini Algiers baada ya biashara za raia wa Misri kushambulia mjini humo.
Maafisa wa shirika la ndege la Misri- Egypt Air na wale wa kampuni ya simu ya Misri wamesema walishambuliwa Jumapili wakati wa maandamano ya kuiunga mkono timu ya taifa ya soka la Algeria.
Maelfu ya watu wamekusanyika wakiwa na matumaini ya kununua tikiti za ndege kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudio baina ya Algeria na Misri siku ya Jumatano.
Mchezo huo wa siku ya Jumatano ndio utaamua nchi ipi kati ya hizo mbili itafuzu kucheza Kombe la Dunia Afrika Kusini mwaka 2010. habari na
BBCSWAHILI.com

MAKAMPUNI 15 YATOA MSAADA KWA JESHI LA POLISI!!

Waziri wa mambo ya Ndani Lawrence Masha kushoto pamoja na Inspekta Generali wa Polisi Saidi Mwema wakisikiliza jambo wakati wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya utendaji kazi kwa jeshi la polisi Dar es Salaam, msaada ni kutoka katika makampuni mbalimbali nchini.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na buti 500, kofia za barret 1000, viatu vya kawaida jozi 200, seti moja ya jezi za mpira wa miguu, seti 1 ya jacketi za riadha, cardon tape mita 10,000, vitabu 400 vya kurekodi taarifa za uhalifu, mikanda ya filimbi 500, gloves 500, key holders 300, reflector 500, stable belt 500, mobile hand set 10 na solar lamp vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia moja kumi na nne, laki sita na thelathini.
Makampuni yaliyotoa vifaa hivyo ni pamoja na Italy Shoes Co Ltd, JM Tredars, Regalia Tanzania ltd, Katwe International Co ltd, Chama cha Riadha Tanzania, Cozy Tredars, Lugumi Interprise Ltd, Digital international, Dry Cell General traders, Open Sanity, Status Investiment, BigBon Petroleum Ltd, Mhonyiwa and Company ltd,Daissy General Traders

Picha ya pamoja ya wawakilishi wa makampuni, waziri Masha na wawakilishi wa jeshi la polisi.


Wanafunzi watoro 594 katika wilaya ya Bahi warejeshwa shuleni na kuendelea na masomo!!

Na Anna Nkinda - Maelezo, Bahi
16/11/2009 Serikali wilayani Bahi mkoani Dodoma imefanikiwa kuwarejesha shuleni wanafunzi watoro 594 kati ya wanafunzi1012 ambao waliacha masomo ya elimu ya msingi na sekondari na kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa wilaya hiyo Betty Mkwasa wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya wilaya kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo.
"Kwa upande wa shule za msingi kulikuwa na wanafunzi watoro 776 wavulana ni 364 na wasichana 412 wanafunzi waliorejeshwa ni 464 wavulana 201 na wasichana 263 na shule za sekondari kulikuwa na watoro 236 wavulana 107 na wasichana 129 waliorejeshwa ni 130 wavulana 74 na wasichana 56", alisema Mkwasa.
Mkuu huyo wa wilaya aliendelea kusema kuwa bado wanaendelea kuwafuatilia wanafunzi wengine waliobaki ili nao waweze kurejeshwa shuleni na kuendelea na masomo yao kwani wanafunzi waliorejeshwa katika shule za sekondari ni sawa na asilimia 55 na shule za msingi ni asilimia 59 tu.
Aliendelea kusema kuwa hivi sasa tatizo la utoro limepungua katika wilaya hiyo kutokana na kufungua shule za msingi mpya nane katika maeneo ya wafugaji yenye watu wengi, shule 23 za msingi zipo katika mpango lishe wa School Feeding Programme (WFP) , mashirika mbalimbali kupitia kanisa la Anglikana kutoa lishe kwa baadhi ya shule na utoaji wa semina na maelekezo ya mara kwa mara kwa walimu wakuu na waratibu elimu kata kuhusu mahudhurio ya lazima.
Kuhusiana na ulipaji wa madeni ya walimu wa wilaya hiyo Mkwasa alisema kuwa Serikali imewalipa walimu 290 Tshs. 112,762,653/= madai ya fedha za uhamisho, masomo, likizo, matibabu na posho ya kujikimu ambayo yaliyohakikiwa mwezi Februari mwaka huu na kulipwa mwezi wa kumi 2009.
Alizitaja changamoto mbalimbali za elimu wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu katika fani za masomo ya sayansi, upungufu wa vifaa vya kujifunza na kujifunzia, miundombinu hafifu katika maeneo ya kazi kama umeme, maji na barabara, upungufu wa majengo yakiwemo madarasa, mabweni, hosteli, vyoo, nyumba za walimu na majengo ya utawala.
Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wanafunzi wa wilaya hiyo kuachana na tabia ya utoro ambayo haitawasaidia kitu chochote katika maisha yao ya baadaye badala yake waende shule.
Mama Kikwete alisema, "ninachowasihi watoto wangu angalieni sana mazingira yasiwatawale bali ninyi ndiyo myatawale mazingira hakika kwa kufanya hivyo mtakuja kufanikiwa katika maisha yenu kwani kuna baadhi ya wanafunzi katika umri wenu wanatawaliwa na mazingira na kujiingiza katika makundi yasiyofaa na hivyo kuharibikiwa kimaisha".
Akiwa wilayani humo Mama Kikwete alitembelea shule ya watoto wenye ulemavu wa kusikia iliyopo Kigwe na kuona jinsi wanafunzi hao wanavyoishi na kusoma shuleni hapo pia aliwapatia zawadi ya Tshs. 500,000/= fedha ambazo watazitumia kununua jezi pamoja na mipira.
Wilaya ya Bahi inajumla ya madasara 68 ya elimu ya awali yenye wanafunzi 6358, shule za msingi 70 zenye wanafunzi 32156 wakiwemo wavulana 16178 na wasichana 15978 na shule za sekondari 20 zenye wanafunzi 3146 wasichana 1346 na wavulana 1800.
Taasisi ya WAMA ilivichangia vikundi vya wanawake wajasiriamali vilivyopo wilayani humo Tshs. 1,500,000/= fedha ambazo zitatumika kuinua mitaji ya vikundi hivyo.
Mwisho.

Mama got Swag!


TBC1 WAPIGWA JEKI NA SERENGETI!!

TAJI LIUNDI(KULIA)-meneja wa timu ya shirika la utangazaji Tanzania (tbc sports club)akipokea jezi kutoka kwa TEDY MAPUNDA-meneja wa uhusiano,habari na mawasilino wa SERENGETI BREWERIES(SBL).msaaa wa jezi juu na chini 20 na mipira mitano.vyote vinathamani ya shilingi laki 8.TBC SPORTS CLUB kwa sasa ipo TANGA ikishiriki michuano ya mashirika ya umma na makampuni binafsi SHIMMUTA.

VIJANA WA TBC1 WAKIKAZA BUTI KAZINI!!

Watangaji wa mpira wa miguu wanaochipukia kwa sasa hapa nchini ENOCK BWIGANE(kulia aliyevaa uzi wa TAIFA STARS)na AHMED SALUM(kushoto)wote wa shirika la utangazaji Tanzania-TBC wakiwajibika katika kutangaza mpira uwanja mpya wa kisasa wa TAIFA jijini DSM.kweli TBC ni shule inayoibua vipaji vipya na vya ukweli katika utangazaji wa mpira nchini.BIG UP TBC na mkurugenzi TIDO MHANDO.

MANJU MSITA NA UBUNIFU WA MAVAZI YA KIAFRIKA!!

Manju Msita mbunifu wa mavazi aliyeshiriki katika maonyesho ya Swahili Fashion Week yaliyomalizika hivi karibuni katika Viwanja vya Karimjee akipita mbele ya wageni waalikwa mara baada ya wanamitindo kupita jukwaani na mavazi yake aliyobuni, baada ya shughuli hiyo kubwa FULLSHANGWE imeongea na mbunifu huyo mahiri nchini na anasema "Nilizaliwa ili nibuni kwani nilipokuwa tumboni mwa mama yangu ndipo hasa nilipokuwa shule, na siku nilipozaliwa ndipo nilipotunukiwa Shahada yangu ya ubunifu"
Kwa kifupi ni kwamba kuna mambo unayakuta duniani na kuna mambo mengine unakuja nayo duniani, kwa suala la ubunifu ni lazima uje nao kwani ni hakuna mtu atakufundisha kubuni na kama itatokea kufundishwa basi utajifunza yale aliyonayo yeye.
Hebu angalia ubunifu huu wa mbunifu Manju Msita uweze kuona kazi zake na uwezo wake katika kubuni mavazi kazi kwako Mdau wa FULLSHANGWE.

Umewahi kuona Mvuvi akiwa ameongozana na samaki hebu angalia ubunifu huu wa Manju Msita ulivyosheheni vitu.

Kumbe gunia likichanganywa na Linen linaweza kumtoa mwanamke bomba kama hivi.

Unaonaje Linen inapochanganywa na gunia unapata picha?
Hii ni ya kiume na imechanganywa kwa kitambaa cha Linen iliyochanagnywa na Kitenge.
Hii nguo imetengenezwa kwa bridal satin na kitenge kama unavyoiona inapendeza ukiitazama.

KAZI YA HESHIMA YA MWANAMUZIKI YOUSSOUR NDOUR!!

Mwanamuziki Youssou Ndour anayeheshimika sana duniani kutoka nchini Senegal akiimba mbele ya mashabiki lukuki waliohudhuria katika onyesho lake pamoja na mwanamuziki wa kike kutoka Benin Angelique Kidjo wakati wa tamasha la muziki la taasisi ya Mohamed Mo lililofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam usiku wa kuakia leo onyesho hilo limekuwa ni changamoto kwa wanamuziki wa hapa nyumbani na afrika pia kwani mwanamuziki huyu amekuwa akitumia vifaa vya kiafrika kama vile Talkingdrum, percussion (ngoma za asili) pamoja na vifaa vingine vya kisasa ambavyo vimekuwa vikitengeneza muziki wenye ladha na midundo halisi ya kiafrika inayokubalika sehemu yoyote duniani na ndiyo maana amekuwa akipata heshima kubwa duniani na hii inadhihirisha kuwa kumbe kuna muziki mwingine mzuri zaidi hata ya muziki wa bolingo kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Hapa Youssou Ndour akiimba kabla mashabiki hawajaanza kupandisha mzuka
Mwanamuziki Anjelique Kidjo akifanya vitu vyake kwenye tamasha la muziki la Ibrahim Mo lililofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

MAMA KIKWETE KATIKA ZIARA WILAYANI BAHI!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amevaa vazi la asili la kabila la wagogo mara baada ya kuvalishwa na wakazi wa kijiji cha Mdemu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.Picha na Juma Kengele - Ikulu
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpima uzito mtoto Jonathani Deogratus mwenye umri wa miezi kumi ambaye alipatikana na uzito wa kilo 11.5 huku mama wa mtoto huo Rosemary Deogratus akimsaidia kuweka kwenye mzani wakati alipotembelea kituo cha afya Kigwe kilichopo wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma.

Mke wa Rais Mwalimu Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akisahihisha daftari la Lea Wimbe ambaye ni mlemavu wa kusikia mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya viziwi Kigwe. Mama Kikwete alitembelea shuleni hapo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani Bahi katika mkoa wa Dodoma

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiongea na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa wilaya ya Dodoma mjini kuhusu kujitokeza kwao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa kijiji cha Kigwe juu ya kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa maralia wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo katika wilaya ya Bhi mkoani Dodoma kwa ajili ya kuwapatia msaada wa vifaa mbalimbali vya afya.

Tanzania yajitutumua tena kwenye maonyesho ya Utalii nchini Uingereza!

Mh. Shamsa Mwangunga katikati akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Utalii nchini waliohudhuria katika maonyesho hayo.
Tanzania imefanikiwa kufanya vyema tena kwenye maonyesho ya Utalii yaliyofanyika nchini Uingereza mwanzoni mwa mwezi huu, Tanzania kwa mara nyingine imeshiriki kwenye maonyesho ya hayo kuanzia tarehe 9 mpaka tarehe 12 November 2009,
Bodi ya Utalii nchini (TTB) ndiyo iliyosimamia kikamilifu ushiriki wa Tanzania klatika maonyesho hao makubwa na maarufu nchini Uingereza, Banda la Tanzania lilikuwa ndiyo kati ya mabanda mazuri na ya kuvutia kati ya nchi washiriki zilizoshiriki kwenye maonyesho hayo.
Jumla ya kampuni binafsi 59 kutoka Tanzania zilikuwepo kuuza vivutio vya Utalii na safari kwa wageni ili kutembelea na kufanya utalii nchini Tanzania, Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Shamsha Mwangunga na baadhi ya maafisa wengine kutoka Tanapa, Ngorongoro na Bodi ya Utalii waliowakiliswa na Mkurugezi Mkuu wa Bodi hiyo Mr. Peter Mwenguo.
Nchi ya Tanzania imeweza kutangazwa kupitia maonyesho hayo makubwa duniani yajulikanayo kama World Traveller Market (WTM) yaliyofanyika katika viwanja vya excel jijini London nchini Uingereza

Sunday, November 15, 2009

WAREMBO MISS EAST AFRICA KUANZA KUWASILI DESEMBA 1-2009!

SELAMAWIT ZERABRUCK GHEBRESLASSIE -18 YEARS (ERITREA)

Warembo wanaoshiriki mashindano ya kimataifa ya MISS EAST AFRICA 2009 wataanza kuwasiri Nchini tarehe moja mwezi ujao kwa ajili ya mashindano hayo yanayosubiliwa kwa hamu kubwa na watu wengi Barani Afrika.
Wakiwa jijini Dar es salaam, warembo hao watafikia katika hoteli ya kimataifa ya Kunduchi Beach Hotel & Resort ambayo ndiyo hoteli rasmi ya mashindano ya Miss East Africa 2009.
Mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 yanatarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi ujao katika ukumbi wa Mlimani City jijini dare s salaam na yatawashirikisha warembo kutoka Nchi 14 za ukanda wa Afrika mashariki ambazo ni pamoja na wenyeji Tanzania,
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Nchi zingine zinazoshiriki katika mashindano hayo ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, pamoja na visiwa vya Seychelles, Comoros, Madagascar, Reunion na Mauritius.
Mashindano hayo yanayoandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam yanatarajiwa kutizamwa na watu zaidi ya millioni 200 kupitia katika Television barani Afrika.
Mrembo Claudia Niyonzima wa Burundi ndiye anayeshikilia taji la Miss East Africa kwa sasa.
AKAZUBA CYNTHIA-20 YEARS (RWANDA)

QUEEN BELLE MONIQUE-23 YEARS (BURUNDI)

ALIDA GROLIA KANEZA-19 YEARS (BURUNDI)

SEFORA MESSELE GHEBREEZGABIHEIR-18 YEARS (ERITREA)

MARRY KIRABO -18 YEARS (UGANDA)

REBEKA GETACHEW-23 YEARS (ETHIOPIA)

AKAZUBA CYNTHIA -20 Y(L)and MAHORO ANNET-23 Y (R)
(RWANDA)

Wazazi wilayani Kondoa watakiwa kusomesha watoto wao

Na Anna Nkinda - Maelezo, Kondoa
Wazazi wilayani Kondoa wametakiwa kuwasomesha watoto wao kwa bidii na kutilia mkazo suala la elimu kwani Ulimwengu wa sasa bila ya kuwa na elimu ya kutosha huwezi kuwa na maendeleo ya maana.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipokuwa akiongea na wakazi wa wilaya hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa hivi sasa kuna umuhimu wa kusomesha watoto wote wa kike na wa kiume bila ya kuwabagua kwani hao ndio watakaokuja kuwatunza hapo baadaye wakiwa wazee.
"Ninawaomba muwahimize watoto wenu wasome kwa bidii elimu Dini na elimu Dunia kwani kama mtoto akiwa na elimu hizi zote mbili atakuwa katika maadili mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu na wanadamu", alisema Mwenyekiti huyo wa WAMA.

Saturday, November 14, 2009

MDAU GEORGE NJOGOPA WA CLOUDS AVUNA STASHAHADA YAKE BAADA YA KULA NONDOOZ!!

Mdau George Njogopa mtangazji wa kipindi cha jicho letu cha Cha Redio Clouds Fm na mwakilishi wa Voice of America VOA nchini naye amehitimu Stashahada yake ya kwanza katika masuala ya Jinsia katika Maendeleo baada ya kula Nondooz katika chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu J.K.Nyerere Kigamboni zamani (Kivukoni) kwa miaka mitatu, Hongera sana Bw. George Njogopa ni kazi ngumu lakini ndo umeshapiga hatua tena kamada.
Sio dhambi jamani hawa walijisikia kuchoka kutokana na mahafali hayo kucheleweshwa kuanza kwani awali yalikuwa yaanze saa sita lakini yalianza saa nane mchana.
Sasatel mzigoni! wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Sasatel kitengo cha mauzi wakitoa huduma ya kuuza simu wakati wa mahafali ya nne ya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu J.K.Nyerere zamani (Kivukoni)Kigamboni leo kutoka kulia ni Serua, Baraka na Hellennwakiwahudumia wateja wao.

Rais Kikwete akagua uharibifu wa nyumba Msoga!!

Rais Kikwete akukagua baadhi ya nyumba zilizoharibiwa vibaya na mvua kubwa iliyombatana na upepo mkali katika kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo hivi karibuni wakati alipotembelea kijiji hicho leo asubuhi.Jumla ya nyumba51 ziliharibiwa vibaya na mvua hiyo na kusababisha watu zaidi ya 190 kukosa makazi na kuhifadhiwa na majirani(picha na Freddy Maro)

Friday, November 13, 2009

Nigeria's little big man!

Dami Paul.

Dami Paul does not cut the most impressive figure between the pipes. Quite short for a goalkeeper, at only 173cm, he looks all at sea in the large white frame of the goal. However, Nigeria's No1 has proven himself to be a top shot-stopper at these finals. His spring-loaded reflex saves kept the Spaniards at bay on two occasions in particular, making him every inch the unsung hero of the crucial 3-1 semi-final win in Lagos.
While sumptuous attackers Sani Emmanuel and Stanley Okoro are the ones grabbing all the headlines in the fawning local media, the soft-spoken net-minder is doing more than his fair share for the cause. "We are a very offensive and aggressive team and we create a lot of scoring chances," the diminutive net-minder told FIFA.com deep in the cement bowels of the Teslim Balogun Stadium. "We can still do a little better at taking our chances and we will need to be a little more clinical in the final," he adds, stoking the fire for his colleagues in attack.
For us, this is the top of world football, the most we can do. We will go out and fight as a team as we have done all the way up to the final.
Nigeria goalkeeper Dami Paul
Spain's finishers had been quite ruthless in their games leading up to the semi with the hosts, scoring a then tournament-best 16 goals. But it took the previously prolific La Rojita a full 83 minutes to finally find a way past Nigeria's athletic and acrobatic net-minder. At that point the game was already beyond the Spaniards thanks, in large part, to a pair of reflex saves by Paul, first on Isco from close range and then from Pablo Sarabia. On both occasions, this spring-loaded little man between the pipes appeared to have thwarted odds-on goals. "I'm really glad to have made these saves, because if they managed to draw level or get an early goal it could have given them confidence."

Bodi mpya ya 8 ya TAFIRI yazinduliwa leo jijini Dar!!

Mkurugenzi wa TAFIRI (katikati) Dr.Yohana Budeba akimueleza Waziri Wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi John Magufuli jinsi ya uhifadhi wa samaki kwenye kabati maaluum leo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya 8 ya TAFIRI..(picha na Mwanakombo Jumaa -Maelezo.)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi John Magufuli(kushoto) akimkabidhi zawadi mjumbe wa Bodi hiyo aliemaliza muda wake Ruth Msafiri (kulia) kaikati ni Mwenyekiti mpya wa BODI ya 8 ya TAFIRI Prof. Yunus Mgaya.
Waziri Wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ( Kulia) akisikiza wakati alipokuwa akipewa maelezo jinsi ya kuhifadhi wa samaki katika majokofu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya TAFIRI Dr. Yohana Budeba (kati) leo katika makao makuu ya taasisi hiyo Kunduchi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya 8 ya TAFIRI.

Naomi Campbell afanya tamasha la mavazi Dar es Salaam!!

Mke wa Rais mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) akimweleza jambo Balozi wa kimataifa wa Utepe na msanii na mwanamitindo wakati wa onyesho la mavazi lililoandaliwa na Taassi ya Utepe Mweupe.
Na Anna Nkinda – MAELEZO
Jumla ya dola za kimarekani 10,000/= zimepatikana kutokana na mnada wa nguo ya kike iliyotolewa na msanii na mwanamitindo wa Kimataifa Naomi Campbell katika maonesho ya mavazi ya Relief Tanzania yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Movenpick jijjini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yaliandaliwa na Naomi Campbell ambaye ni Balozi wa Kimataifa wa Utepe Mweupe kwa kushirikiana na Mustafa Hassanali ambaye ni mwanamitindo wa hapa nchini kwa lengo la kukusanya fedha ili kutunisha mfuko wa Mtandao wa Utepe Mweupe (The White Ribbon Alliance).
Akiongea mara baada ya maonesho hayo Campbell alisema lengo la kufanya maonyesho hayo ni kupata fedha ambazo zitatumika katika kampeni ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Kuhusu wabunifu wa mavazi na wanamitindo wa hapa Tanzania alisema anaridhishwa na kazi zao na wanajitahidi kufanya kazi nzuri kwa ufasaha mkubwa na kwa kujituma.
Aliendelea kusema kuwa anaipenda nchi ya Tanzania kwa sasabu inavivutio vingi kama vile mbuga za wanyama, visiwa vya Zanzibar, mito, milima, maziwa na Bahari ya Hindi huku akisisitiza kuwa si mara ya kwanza kuja Tanzania na ana wa kuendelelea kuja hapa nchini.
Katika maonyesho hayo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Banda walihudhuria.
Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon Alliance) wenye takribani nchi wanachama 143 duniani ambao jana uliadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake unafanya kazi kubwa yakuhakikisha kuwa nchi wanachama zinaondokana na vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

FIESTA 2009 ONE LOVE ONDOKA NA HUU MCHUMA!!


WHO YAMWAGA MISAADA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII!!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akizungumza mbele ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari wakati Wizara hiyo ilipokabidhiwa msaada wa magari, Pikipiki na vifaa mbalimbali na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Dr. Jean Baptiste Kapko katika ofisi za wizara hiyo mtaa wa Samora leo, vifaa vilivuyokabidhiwa kwa Wizara na shirika hilo ni Magari 14 ya kubebea wagonjwa aina ya Toyota Landcruser, magari mengine 5 aina ya Toyota Pickup,Pikipiki 5, Kompyuta za mkononi , Jokofu la Kuhifadhia Damu na mashine ya Kurudufu (Photocopy Machine) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.3 sawa na dolla za Kimarekani 985,718, Shirika hilo la afya Duniani limetoa msaada huo katika wakati muafaka kutokana na matatizo mengi yanayoikwamisha sekta ya afya kutoa huduma hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali kupitia wizara yake ya Afya na Ustawi wa Jamii, kushoto kwa waziri ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Aisha Kigoda.
Waziri Mwakyusa kulia Akipokea msaada wa moja ya magari 14 ya kubebea wagonjwa aina ya Toyota Landcruser yaliyokabidhiwa kwa Wizara hiyo na mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Dr Jean Baptiste Tapko katika makao makuu ya Wizara hiyo.
Waziri Mwakyusa hapa akiangalia moja ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa Wizara na Shirika la Afya Duniani (WHO) leo anayeangalia kushoto ni Naibu waziri wa wizara hiyo Aisha Kigoda.
Waziri Mwakyusa akiangalia mashine ya kurudufu (Photocopy Machine) mara baada ya kukabidhiwa leo.

Waiziri wa Afya Prof. David Mwakyusa wa sita kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea msaada huo leo.

NAOMI CAMBELL KATIKA JUKWAA LA MITINDO TANZANIA!!

Naomi Cambell akifanya vitu vyake jukwaani wakati wa onyesho maalum lililoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya The White Ribbon Alliance for Safe Motherhood (WRA) nchini lililofanyika jana kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa kuamkia leo kama kampeni ya kuhamasisha afya kwa mama na Mtoto mara baada ya mzazi huyo kujifungua

Mtangazaji wa East Africa Televition Deogratius Kithama akifanya mahojiano na mwanamitindo Naomi Cambell usiku wa kuamia leo.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiongea na Mwanamitindo wa kimataifa Naomi Cambell wakati wa onyesho la mavazi la The White Ribbon Alliance for safe Motherhood lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa kuamkia leo taasisi hiyo inajishughulisha na kampeni ya uzazi salama kwa wakima mama wajawazito katikati ni mwanamitindo wa Face Of Afrika kutoka Zimbabwe Tollar Kelle, kushoto ni Franco Tramontana na kushoto ni Mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali.

Thursday, November 12, 2009

MAMA SALMA KIKWETE NA MAMA THANDIWE BANDA KATIKA MKUTANO WA UTEPE MWEUPE LEO!!

Mke wa Rais mama Salma Kikwete(katikati) akiwa na Mke wa Rais wa Zambia mama Thandiwe Banda (kushoto) pamoja na mke wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu mama Anna Mkapa wakishiriki mkutano mkuu wa mwaka wa kimataifa wa Taasisi ya Utepe Mweupe leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo unaowashirikisha wanachama kutoka nchi zaidi ya 20 pamoja na mambo mengine unajadili uzazi salama kwa wanawake na njia bora za kupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua

Pulling Strings for 2010

With such a large number of people coming to South Africa next year and with the attention that the country will receive during the 2010 FIFA World Cup™, it is the perfect opportunity for South Africans to showcase their talent and explore the business potential of such a mega-sporting event.
One South African is doing just this with his unique – and large – brand of puppetry which will no doubt have the crowds in awe as they are entertained by more than just the action on the pitch.
Daniel Popper is a young artist working and teaching in Cape Town. It was only after graduating from the University of Cape Town’s Michaelis School of Fine Art in 2006 that he first began manufacturing his massive artworks. Over the space of two years, working through trial and error, and a few hints from the internet, he slowly began a process that would lead to the enormous puppets he has now completed.
“When I made my first puppet it was for fun, an experiment. Since then I've taken various puppets to festivals and gatherings where people kept saying how lots of these would look amazing together on a field, at an event, so I came up with this idea to make giant soccer players for the World Cup,” says Popper.
These massive puppets stand at over five metres tall, almost big enough to look through a second floor window. The necessarily lightweight frame is manufactured out of a number of materials, from fabric and bamboo, to aluminium and foam. Each one of these giant structures is operated by a single puppeteer who is strapped into a harness below the puppet. Included in the puppet’s intricate design is a lighting system, which allows the giant art-forms to shine at night, changing their appearance and making their already incredible presence even more commanding.
Popper feels that these puppets offer people something special to the audience watching them. “The attraction is that they are giant; it is always eye catching to see something this big. While a lot of entertainment today is static and boring, these puppets move, they dance, and because of this they really capture people's imagination. They take people out of their environment for a moment, and they start to relax because the puppet reminds them that they are out to have fun,” says Popper.
Since last year Popper's aspirations for the tournament have grown, and he has been encouraged by the response to his prototypes. “It would be amazing if they could be all over the place,” he said, obviously excited for the influx of 450,000 expected visitors next year, many of whom will get to witness his puppets in action on the streets of Cape Town and other cities around South Africa.
Now running his own business, Popper credits the arrival of the 2010 FIFA World Cup for playing a big part in inspiring him to become an entrepreneur “I think that there are opportunities for everybody, but for creative people especially. For a lot of the artists in the country now is a chance for them to put their work out there for the rest of the world to see. This is history and we as artists can record that.”
His advice for other people looking to start up their own businesses ahead of the tournament next year? “Just go for it, don't be afraid to do it. It is tough but the opportunities are there, just be properly prepared.”
The giant football puppets will be performing for the first time at the friendly match between South Africa and Japan at the newly completed World Cup stadium, Nelson Mandela Bay , in Port Elizabeth on Saturday 14 November.

ELIZABETH GUPTA AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI!!

Aliyekuwa mshiriki wa Bigbrother Revolution Elizabeth Gupta akiongea na wanahabari sasa hivi katika mkutano unaoendelea kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar es salaam, Elizabeth alirejea jana kutoka afrika Kusini baada ya kuishi katika jumba hilo kwa siku 63 na baadaye kupigiwa kura ya kutoka nje na washiriki wa shindano hilo pamoja na mashabiki,
Elizabeth amesema anashukuru kwa kupata nafasi hiyo kwani amejifunza mambo mengi lakini pia anaweza kupata mafanikio mengine mengi kutokana na ushiriki wake katika shindano la Bigbrother Revolution na anaamini kwamba wasichana wengi watakuwa wamejifunza mengi kupitia kwake pia ameomba radhi kama kuna mashabiki aliwaudhi kwani katika maisha ya kila siku kwenye jumba hilo sio rahisi kumfurahisha kila mtu.
Meneja Huduma wa Multchoice Ronald Shelukindo akizungumza na wanahabari wakati wa kumkaribisha Elizabeth Gupta katikati ili aongee na wa aandishi wa habari katika mkutano unaoendelea kwenye Hoteli ya Paradise City jijini Dar mara baada ya kurejea jana kutoka Afrika kusini.

U N I T E D N A T I O N S P R E S S R E L E A S E

Nelson Mandela.
On Tuesday, 10 November 2009, the UN General Assembly adopted, without a vote, draft resolution A/64/L.13, introduced by South Africa on the Nelson Mandela International Day.
The resolution recognizes the long history of Nelson Rolihlahla Mandela’s leading role in and support for Africa’s struggle for liberation and Africa’s unity, and his outstanding contribution to the creation of a non-racial, non-sexist, democratic South Africa, as well as Nelson Mandela’s values and his dedication to the service of humanity as a humanitarian, in the fields of conflict resolution, race relations, promotion and protection of human rights, reconciliation, gender equality, the rights of children and other vulnerable groups, as well as the uplifting of poor and underdeveloped communities.
The General Assembly decided to designate 18 July as Nelson Mandela International Day, to be observed each year beginning in 2010.
The President of the General Assembly, Ali Abdussalam Treki, expressed “appreciation to this great man who dedicated his life and suffered for the sake of man everywhere”. Dr. Treki paid tribute to the fighter and his struggle, to what Nelson Mandela had achieved.

Wednesday, November 11, 2009

MSHIRIKI WA BIGBROTHER REVOLUTION ELIZABETH GUPTA AREJEA!!

Mshiriki wa Bigbrother Africa Revolution Elizabeth Gupta katikati akitoka katika uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere jana jioni mara baada ya kuwasili akitokea afrika kusini ambako alikuwa kishiriki katika shindano la Bigbrother Revolution kulia ni mama yake mazazi Bi. Hellen Gupta salaam kushoto ni Ronald Shelukindo Meneja huduma wa Multchoice Elizaberth alitolewa katika jumba hilo jumapili iliyopita baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa shindano hilo na wenzie, matukio zaidi tutakuletea kesho.

Elizabeth akipozi kwa picha mbele ya walinzi wake baada ya kupokelewa

Elizabeth Gupta akiwa na mtoto wa ndugu yake anayeitwa Upendo Nick But aliyejumuika pamoja na ndugu na mashabiki katika mapokezi hayo
Jamani Elizaberth Full Mapozi kwenye picha.
Huu ndiyousafiri uliomchukua Elizaberth

Mdau Jackson Kalikumtima alikuwepo pia na watoto wake kama unavyowaona

Mamaa Ennet na mtoto wake Upendo walikuwepo kumpokea ndugu yao Elizabeth

Mwinyi wa Machozi Band na Aminata wakipozi kwa picha nao walikuwepo katika uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere kumpokea Lady Jaydee lakini pia wakajumuika amoja na mashabiki wengine katika kumpokea Elizabeth Gupta.

MWISHO WA KUSAJIRI NAMBA ZA SIMU NI DESEMBA 31, 2009!!

Waziri wa Elimu ya juu Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msola akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katika mtaa wa Jamhuri wakati alipozungumzia juu ya watumiaji wa simu za mkononi kusajiri na mba zao za simu, amesema mwisho wa zoezi hilo la kusajiri namba za simu utakuwa Desemaba 31 mwaka huu kazi kwenu wanamitandao.

DARASA LA NNE KATIKA MITIHANI LEO NA KESHO!

Wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Maktaba ya jijini Dar es salaam wakiondoka shuleni kurudi nyumbani mara baada ya kufanya mtihani wao leo kabla ya kuingia darasa la tano mwakani, ambapo mtihani huo umefanyika kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini na utafanyika kwa siku mbili mfululizo leo na kesho.

Grizzlies rookie Thabeet leaves game with broken jaw

Memphis Grizzlies rookie center Hasheem Thabeet, the second overall pick in the June draft, left Tuesday night's game against the Portland Trail Blazers with a broken jaw.
The 7-foot-3 center from UConn was injured late in the first quarter during a battle under the Memphis basket. Replays appeared to show Thabeet's jaw colliding with forward Zach Randolph's head.
Thabeet had just entered the game a minute earlier.
Thabeet was playing in his seventh game of the season. He had scored four points and grabbed 11 rebounds in his previous six games, and also recorded six blocks.
story by www.nba.com

Rais Kikwete akutana na wanafunzi Cairo!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini Misri baada ya kukutana na kuzungumza nao mjinji Cairo,Misri jana jioni(picha na Freddy Maro)

President Kikwete inspects agricultural activities in Egypt!!

The chairperson of the Magrabi Agriculture Company Mr.Sherif El Maghraby shows President Jakaya Mrisho Kikwete some of his farm produce being processed for export when the president visited the farm yesterday evening in Nobaria area North Cairo.Magrabi Farms one of the Egypt’s land reclamation private investment projects has a total of 7,630 acres. Some of the farm’s produce include quality letuce, banana, strawberry, grapes and some vegetables and herbal varieties (photos by Freddy Maro)


CLUB MAISHA "HAYA NI MAISHA" MAMA HELLEN SWEYA

The Director of Club Maisha Hellen Sweya addressing the press during the press Conference at Club Maisha today
On the 8th November 2009 at around 14 hrs a fire was detected in the Maisha VIP area by our good neighbours and pesnnel on duty. when iti became apparent that they wpuld not be able to successfully extinguish the rapidly spreading fir. they immediately called in the police Kinondoni Region Dar es salaam city fire service Knight Support, Group4 as well as Tanesco to switch of the power nertwork in the area.
With Lots of courage from the fire service departments CLUB MAISHA employees and neighbours the fire was contained at around 6.30 pm to the extensive destructionof everything that was in the club, it is with luck that no injury to both the fire tenders and CLUB MAISHA employees and neighbours was recorded.
The couse of this damaging is still unknown and at current CLUB MAISHA management with the help of experts is establishing the extent of damage to property and stock.on behalf of CLUB MAISHA Management and staff we would like to thank all individualswho have gone beyond the call of duty in helping us, in particular Dar es salaam City Fire Service Knight Support , Gropu4 Security, TANESCO, Kinondoni Region Police Force,Oysterbay ward Leadership, our neighbours and the press and not to forget friends, family members and all best wishers who sent us massages of encouragement and sympathy.
We shall continue to give an update of developments as more findings unford.

MAISHA YANAENDELEA

IBUA FILMS STAR TANZANIA YAHAMIA MWANZA

Majaji wakishoo love na yale madini yatakayowakilisha jiji la A-town.

Baada ya mchakato mzima wa kuibua vipaji vya wasanii chipukizi wa maigizo yaani IBUA Film Star Tanzania kuanzia Arusha, zoezi zima linahamia Mwanza katika Nyanza Shule ya msingi iliyopo Balewa Road tarehe 14 na 15 Novemba kabla ya kuhamia Dodoma.
Chipukizi waliofanikiwa kuiwakilisha mkoa wa Arusha ni pamoja na Salum Ahmed Shafii, Pauline Edward Munisi, Michael Elias Mrema, Mbara Meena na Enhard Haruna. Kutokana na mwamko mkubwa wa wasanii chipukizi, fomu za kujiunga na shindano la IBUA Film Star Tanzania zinaendelea kutolewa maeneo mbali mbali na mikoa husika. Hii ni kuwawezesha wasanii chipukizi kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ya kuendeleza vipaji vyao na kuviacha vikipotea kwa kukosa njia ya kuvikuza. Usaili wa mikoani utaandaliwa vipindi maalum na kuonyeshwa kupitia mojawapo ya runinga hapa nchini.
Taasisi ya YEC Production, inayojihusisha na kukuza na kuibua vipaji kwa vijana katika ulingo wa filamu nchini, imegundua njia pekee ya kuibua vipaji hivyo na kuviokoa visipotee kwa kuanzisha shindano maalum la kusaka vipaji. Washiriki wataonyeshwa kwenye runinga kupitia kipindi maalum ambapo watazamaji watahusishwa kumpata staa halisi wa filamu Tanzania.
Mbali na kuviendeleza vipaji vyao pia washiriki watapata mafunzo katika nyanja zote kuanzia za uandishi wa muongozo (scripting) hadi uigizaji bora na kuwawezesha kufikia malengo yao.
Vigezo vilivyotumika katika kumsaka msanii huyo chipukizi ni kuwa na umri wa miaka 16 ikiwa ni pamoja na uelewa. Hata kutokuonekana katika tamthilia au sinema ya aina fulani hapa nchini hicho pia ni kigezo kimojawapo ambacho ni kizuri, kwani vijana wanaochipukia ndiyo wanahitaji msaada mkubwa katika kuibuliwa vipaji, tofauti na wakongwe ambao tayari wamejitangaza.
YEC, imeahidi kuyaangalia matatizo yanayowakabili wasanii kwa kina na kuahidi kutoyarudia, kama yanavyofanywa na baadhi ya wasanii wakongwe, ndiyo maana wameamua kuingia mikataba ya mwaka mmoja na washindi watakaofika kumi bora, ili kuliepuka tatizo hilo.
Sambamba na mikataba hiyo kwa watakaofika kumi bora, pia watatoa nafasi ya kuwapeleka shule watakaoingia tano bora kwa ajili ya kujiendeleza mambo mbali mbali ya sanaa ambapo atakayeibuka kinara atapewa zawadi nyingine maalum.
Pia mchakato wa kuwapata washindi kumi hadi tano bora utaanzia kwenye 20 bora, ambapo watacheza filamu mbili huku majaji wakiangalia kipaji cha msanii mmoja baada ya mwingine na kuendelea kuchujwa hadi kupatikana mshindi.
Filamu watakayocheza zitakuwa katika mandhari ya mtanzania halisi, huku asilimia 60 ya mauzo ya kazi hizo yatakayopatikana zitakuwa kwa ajili ya wasanii wenyewe.
Kutokana na kuona umuhimu wa suala hilo, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) liliamua kutoa vibali halali vya kuendesha mchakato huo, ikiwa ni pamoja na kupewa baraka na chama cha hakimiliki Tanzania (COSOTA) ya kusimamia kazi hiyo.
Mikoa husika katika mchakato wa kwanza ni Arusha, Mbeya, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam lakini wigo wa mikoa utaongezeka mwaka hadi mwaka.

Tuesday, November 10, 2009

SUMATRA YATEUA WAKALA WA UKAGUZI WA UTEKELEZAJI WA MASHARTI YA LESENI ZA USAFIRISHAJI ABIRIA MIJINI

Mkurugenzi mkuu wa Sumatra Israel Sekilasa.

Katika kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma za usafiri na kuondoa kero kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Mjini (SUMATRA) imeteua Kampuni ya Majembe Auction Mart kuwa wakala wake wa kufuatilia utekelezaji wa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria kwa mabasi yanayotoa huduma ya usafiri katika Mkoa wa Dar es Salaam (Daladala) na pia mabasi ya Mikoani yanayoanzia Kituo Kikuu cha Ubungo.
Kampuni ya Majembe Auction Mart ambayo imeteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja itatekeleza majukumu waliyopewa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani. Moja ya majukumu makubwa ya Kampuni hiyo itakuwa ni kusimamia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa mabasi ya Daladala yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake ili kuhakikisha kuwa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria yanafuatwa na watoa huduma ili hatimaye huduma ya usafiri katika Jiji iwe bora na yenye kukidhi mahitaji na matarajio ya wakazi wa Dar es Salaam.
Ili huduma ya usafiri katika Jiji iendelee kuwa bora zaidi, ni matarajio ya Mamlaka kuwa wamiliki, madereva pamoja na makondakta wa mabasi ya Daladala watatoa ushirikiano unaostahili kwa Majembe Auction Mart na Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wa utekelezaji wa majukumu yao. Aidha wadau na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka zinazosimamia usafiri pamoja na Kampuni ya Majembe kwa lengo la kuimarisha usimamizi na kuboresha huduma hii muhimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mamlaka ya SUMATRA itafuatilia na kusimamia kwa karibu sana utendaji wa wakala Majembe Auction Mart kwa mujibu wa Sheria na Taratibu ili kuondoa kero za usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Tuchukue fursa hii pia kuwakumbusha wananchi kupunguza purukushani kwa kupanga mstari wakati wa kupanda mabasi.

President Kikwete meets President Mubarak in Cairo!!

president Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with his host President Hosni Mubarak at Cairo Presidential palace yesterday.President Kikwete is in Cairo for the China Africa Cooperation conference(photo by Freddy Maro)

Benitez: We can still win title

Liverpool manager Rafael Benitez.

Liverpool manager Rafael Benitez refused to concede that the title is out of his side's reach despite being 11 points adrift of Premier League leaders Chelsea after a 2-2 draw with Birmingham on Monday.
The Reds have won just one in nine and went into the game against the strugglers on a run of six defeats in eight games. Even though the miserable run continued - and Yossi Benayoun and Albert Riera were added to Liverpool's injury list with hamstring tears - Benitez insists he is not troubled by the bigger picture.
"I think that for the last three weeks to a month, it's been the same," said Benitez. "We only think about one game at a time so I can't talk about anything else, just three points, so I won't talk about the table or positions.
"We won six games in a row before and when we were under pressure we won against Manchester United, playing really well and the character has been fantastic but we couldn't achieve the three points against Birmingham."
Injury concernsBenitez has acknowledged that Liverpool's poor luck with injuries has been a key part in their poor start to the season. Fernando Torres was absent against Birmingham with a groin problem and remains doubtful for the game against Manchester City after the international break, having been withdrawn from Spain duty.
As well as Benayoun and Riera, Benitez also revealed that Danish defender Daniel Agger was struggling with a back problem to even taint the good news of Steven Gerrard coming off the bench to score from the spot after a groin problem of his own. But Benitez is hoping that the international break will finally bring some good news on the injury front, which should lead to an improvement in results.
"We have some players here and we can work with them but there's a difference in match fitness and to be available," said the 49-year-old. "Torres had no confidence so he couldn't play so he's started his treatment. He has to work with physios and try to improve and be ready so we are not talking about an operation, we are talking about treating him properly.
"It's not a deadline so it's a case of seeing how he reacts every day. After the international break, we will see. At least we have Gerrard and Alberto Aquilani coming back and maybe three or four more will be available. We can manage maybe a little bit better."
Birmingham manager Alex McLeish was delighted with his team's display at Anfield, and particularly with a first goal in English football for Ecuador forward Christian Benitez. "Chucho is a handful and it'll do him the world of good," said McLeish. "As they say, you wait ages for a bus to come along and loads come along and hopefully that'll be the case for Chucho and Cameron.
"We'll maybe look back and think we'll never have a better chance of getting three points at Anfield. If we can marry his (Chucho) culture to ours then we've got a superb wee player there. It's a little alien to the game he played in and he's got to get used to that and realise that everyone means the best for him. He's adapting well."
story by www.fifa.com

(Tetesi za Mwanabidii) askari wa usalama watoa sticker maalum baada ya ukaguzi wa gari lenye fire extinguisher!!

Nimesikia tetesi kwamba police wa usalama barabarani wanatoa sticker za kuthibitisha kwamba gari yako imekaguliwa na unacho kizimia moto (fire extinguisher)kwa gharama ya 20,000 kila gari, lakini hiyo bei ni tofauti na manunuzi ya kifaa chenyewe. sasa swali linakuja ....Huu sio ufisadi ? maana siku chache tu kulikuwa na wiki ya usalama barabarani ambapo magari yetu yanakaguliwa na kuhakikisha kila kitu kinafanya kazi na kisha tunapewa inspection report ambayo inajumuisha na hiyo fire extinguisher sasa iweje tena kuwepo na kitu kama hicho ?

Mwenye habari kamili tunaomba utufahamishe tupate uelewa
Joseph Lyimo.

Monday, November 9, 2009

WAKALI WA ZOUK TANZANIA MPO TAYARI? (AMANIWETU) ANAKUJA

Msanii mpya wa mahadhi ya muziki wa ZOUK anayekuja juu kwa kasi ya ajabu zaidi ya kimbunga cha TSUNAMI,ni zao jipya kutoka Nyanda Za Juu Kusini nazungumzia wilaya ya Njombe ndani ya mkoa wa IRINGA
Msanii huyu anajulikana kwa jina la kisanii AMANIWETU jina lake halisi ni AMANI SAID KILLO,anaingia kwenye ulingo wa Zouk akijitambulisha na wimbo wake mpya uitwao 'MAPENZI NI ZAWADI' ikiwa ndio maandalizi ya Album yake ya kwanza itakayokwenda kwa jina la MOYO FICHO LA SIRI.
Msanii huyo amesharekodi nyimbo nne katika studio ya SOUND POWER chini ya Producer B Jayzee(THE PROVIDER) studio hiyo ipo Njombe mjini, kazi ambazo amesharekodi ni pamoja naMAPENZI NI ZAWADI,RAFIKI,MOYO FICHO LA SIRI na WAUZA SURA na kazi nyingine mpya inayopikwa jikoni kwasasa inaitwa NIMEMPATA,Hivyo anaomba wapenzi wa muziki wa Zouk wakae tayari kwani mwanzoni mwa mwaka 2010 album yake itakuwa sokoni

BENDERA YA TAIFA JUU YA MLIMA KILIMANJARO!!

Hizi ni picha za shujaa Elly Gerald Minja, mwanamichezo mwenye uzoefu wa kupanda Mlima wa Kilimanjaro mara baada ya kuifikisha Bendera ya taifa kwenye kilele cha mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika juzi Jumamosi, ikiwa ni katika kuhitimisha mbio za Bia ya Kilimanjaro zilizobeba kampeni ya "Fikisha Tanzania Katika Hatua ya Juu" ikishirikisha wamariadha nyota zaidi ya 70 waliokimbiza bendera kwa zaidi ya kilomita 567 kwa siku tano kuanzia Dar es Salaam hadi Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Elly Gerald Minja akiwa pamoja na wenzake kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro mara baada ya kufikisha bendera ya Taifa kileleni hapo.

Tamasha la Wiki ya Mitindo ya Kiswahili (Swahili Fashion Week) lamalizika!!


Akizungumzia wiki ya mitindo mwaka huu iliyopewa jina la (Swahili Fashion Week)muasisi na muandaaji wa tamasha hilo Mustafa Hassanali alisema kuwa amefurahishwa sana na bunifu mwaka huu na onyesho hilo na anategemea kuandaa onyesho lililo bora zaidi mwakani.
“Nimefurahishwa sana na sapoti tuliyopata kwa wiki ya Mitindo ya Kiswahili, tumekuwa na siku tatu za maonyesho ya mavazi tukiwa na ukumbi uliyojaa watu. Napenda kuwashukuru sana wote waliowezesha kufanikisha maonyesho ya mwaka huu. Napenda kuwashukuru wabunifu wote walioshiriki na wanamitindo walifanya kazi yao vizuri jukwaani. Mwaka huu tumekuwa na wabunifu wazuri na onyesho zuri zaidi na nina shauku kubwa kuandaa Wiki ya mitindo ya Kiswahili mwaka ujao, aliongeza Hassanali.
Katika siku tatu za maonyesho hayo ya mavazi zilizojumuisha wabunifu kutoka ndani na nje ya nchi, pia kulikuwa na onyesho la mabadiliko ya hali ya hewa na tuzo ya mbunifu mpya ya WAPI vilivyodhaminiwa na British Council Tanzania.
Katika tuzo za mbunifu mpya za WAPI , nafasi ya kwanza ilichukuliwa na 2jenge Afrika Matalay, while second place was taken by Kim Dean and third prize went to Diana Hinji.
Siku ya mwisho ya maonyesho hayo ya mavazi pia kulikuwa na tuzo nyingine kama mgeni mualikwa aliyependeza zaidi ambaye alipata malazi ya bure kutoka nyumba ya Swahili Fashion 2009 Southern Sun Hotel na mshindi alikuwa Caroline ambaye ni mwandishi wa magazeti ya Tanzania Standard.
Tuzo nyingine ilikuwa ni ya mwanamitindo bora wa Wiki ya Mitindo ya Kiswahili 2009 ambayo ilichukuliwa na Victoria Martin kwa kuwa mwanamitindo aliyefanya kazi ya visuri kuliko wote.
Katika wiki hiyo ya mitindo, wabunifu wote walipata mafunzo kutoka kwa walimu wa chuo cha ubunifu Munich nchini Ujerumani kupitia warsha ya siku tatu iliyodhaminiwa na Goethe-Institue Tanzania.
Wabunifu walioshiriki katika wiki ya mitindo ya Kiswahili mwaka huu ni pamoja na Manju Msitta, Ailinda Sawe, Farouque Abdela, na Tanzania Mitindo house na wabunifu wageni watakuwa ni Dorothy Lubega wa Uganda na Vaishali Morjaria kutoka Kenya walioonyesha ubunifu wao siku ya tarehe 4 mwezi huu.
Siku ya Alhamisi tarehe 5 Novemba ilianza kwa onyesho la mabadiliko ya hali ya hewa linalodhaminiwa na British Council, likafuatiwa na maonyesho ya mavazi kutoka kwa Farha Naaz, Kemi Kalikawe, Virginia Njumba na Christine Mhando kutoka Tanzania na Vera Vee wa Kenya na Adelia na Sheila Tique wa Msumbiji.
Siku ya Ijumaa iliaanza kwa wabunifu waliokuwa wanawania tuzo ya mbunifu mpya ya WAPI iliyodhaminiwa na British Council ikafuatiwa na maonyesho mavazi kutoka kwa Khadija Mwanamboka, Zamda George, Robi Morro na Fatma Amour kutoka Tanzania na John Kaveke kutoka Kenya na kumaliziwa na mmoja wa wabunifu maarufu barani Afrika David Tlale wa Afrika ya Kusini.
Maonyesho ya Swahili Fashion Week mwaka huu yaliletwa kwa ushirikiano na kampuni za Vodacom Tanzania na ZTE na malazi ya wageni wa SFW kutolewa na Southern Sun Hotel.

TUNAWAJALI GROUP KUANDAA KONGAMANO LA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI!!

Mwenyekiti wa Bw. Abeid Chembe kulia akizungumzia kongamano la kupunguza ajali za barabarani katika mkutano na wanahabari leo
AmesemaTunawajali Group kwa kudhaminiwa na Sameer Africa Tanzania Ltd (YANA) wameandaa kongamno la utafiti wa vyanzo vya ajali za barabarani Tanzania ili kuitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa jamii ambapo alisisitiza matumizi mazuri ya barabara,
hasa zilizojengwa na zinazojengwa kwa kiwango cha lami huku akiomba mwendo kasi wa mabasi na magari mengine uachwe na kuwepo na milango ya dharura katika mabasi na watu waache kuvamia na mambo mengine mengi ambayo yamekuwa yakipelekea kutokea kwa ajali barabarani
Bw. Abeid Chembe amesema wamewafuata wadau mbalimbali kama vile makampuni ya usafirishaji, yanayouza magari, matairi chuo cha usafishaji na wengine wengi ili kuchangia na kufanikisha kongamano hilo ambalo maandalizi yake yanaendelea na tarehe ya kufanyika kwa kongamano hilo itatangazwa wakati wowote kuanzia sasa
Kongamano hilo litazinduliwa hapa jijini na linatarajiwa kufanyika karibu nchi nzima ili kuhakikisha elimu hii ya kupambana na ajari za barabarani inaenea kote nchini

JOHN JAMBELE KUMVAA MAKONGORO MAHANGA UKONGA 2010!!

Bw. John Jambele akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Ukonga kweny uchaguzi ujao 2010.
Bw. John Jambele akiwa na mke wake na mtoto wao mdogo wakati alipokuwa akiongea katika mkutano na waandishi

Bwana John Jambele akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotangaza nia yake ya kumvaa mbunge wa jimbo la Ukonga Mh. Makongoro Mahanga Kada huyo wa CCM amewaeleza waandishi wa habari kuwa
"Mimi John Jambele napenda kuwafahamisha wanaCCM wa mjimbo la Ukonga kuwa mwaka 2010 bunge la jamhuri litakapovunjwa rasmi na majimbo yote nchini kuwa wazi, endapo mungu atanijalia uhai, afya njema nguvu na uzima mara chama cha mapinduzi kitakapotangaza mchakato wa wana CCM kuchuklua fomu za kugombea ubunge na hatimaye kuelekea kwenye kura za maoni ninatarajia kuwa mmoja kati ya wana CCM watakaochukua fomu na hatimaye kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni kwa ajili ya kuwapa fursa wana CCM wa Jimbo la Ukonga kumpendekeza mmoja kati yetu kuwa mgombea wao kabla ya kupelekwa kwenye ngazi za juu zaidi za chama cha mapinduzi kwa ajili ya kuthibitishwa".
Jambele Ameongeza kuwa "Nimeamua kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao 2010 kwa sababu Nia ninayo, Uwezo ninao,na Sababu za msingi ninazo, Nimesema ninao uwezo kwa sababu kwanza ni haki yangu ya kikatiba kabisa ndani ya chama cha mapinduzi na katiba ya nchi ambapo inatamkwa kwenye katiba ya CCM kuwa kila mwanachama hai wa chama cha mapinduzi mwenye akili timamu umri wa kuanzia miaka18 na kuendelea na mwenye sifa zilizoainishwa kwenye katiba anayo haki kuchagua au kuchaguliwa".

Giraffe watia mkono ziara ya Ferre Gola!!

Mwanamuziki Ferre Gola

Timu ya Ferre ikiwajibika jukwaani.

Hoteli ya Giraffe Ocean View ya jijini Dar es salaam imejitokeza kudhaminiziara ya mwanamuziki kutoka Kongo Ferre Gola.Akizunguza meneja mkuu wa hotel hiyo mjini Dar es salaam, Nayak S.K. Rahulalisema “Tumejitolea kudhamini ziara ya Ferre Gola kutoka Kongo ambapojukumu la malazi pamoja na chakula kwa yeye pamoja na wanamuziki wakeitakuwa juu yetu”.Alisema kuwa mwanamuziki huyo mahiri ataweka makazi yake katika hotelihiyo kwa siku zote ambazo atakuwepo mjini Dar es salaam.
Giraffe wamekuwa miongoni mwa wadhamini wa mwanzo kabisa wa ziara hiyoambayo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es salaamkwa mwaliko wa kampuni ya New Habari (2006) ikushirikiana na NYProduction.
Mbali na ziara hii hotel ya Giraffe pia imekuwa ikidhamini ziara namaonesho mbali mbali nchini ikiwemo Miss Tanzania.

Mwenzingo atumbuiza K-mondo

Rashid Mwenzingo akitumbuiza sambamba na wana K-mondo

Aliyekuwa mwanamuziki wa bendi kadhaa za muziki nchini ikiwemo TOT,DoubleM Sound na nyinginezo Rashid Mwenzingo wikiendi hii aliwasilimia kisaniiwanamuziki wa bendi ya K-mondo sound waliokuwa wakitumbuiza katika ukumbiwa Triz Motel uliopo Mbezi jijini Dar es salaam.Mwenzingo aliingia ukumbini hapo kwa lengo la kuangalia shoo hiyo kamawashabiki wengine wa K-mondo lakini alijikuta anapanda jukwaani baada yakukunwa na moja ya vibao vilivyopigwa na bendi hiyo ambavyo vinginealiwahi kuviimba katika bendi alizowahi kufanyia kazi.Mwenzingo ambae kwa sasa anaimba katika bendi ya Msondo alipanda jukwaanihapo na kuimba sambamba wana Kmondo kama ishara ya salam kwa wasaniiwenzake wa bendi hiyo.“Kama ilivyo kawaida yetu wasanii huwa tunasalimiana kisanii”alisema.Bendi ya K-mondo ambayo hufanya maonyesho katika ukumbi huo wa Triz uliopoMbezi kila siku ya Ijumaa inaongozwa na Richard Mangustino sambamba nawanamuziki wengine akiwemo Vumi, Toto Tundu ‘ Panduka’ na wengineo.

President Kikwete meets chinese Prime Minister!!

President Jakaya Mrisho Kikwete meets the Chinese Prime Minister Wen Jiabao at Sharm el Sheikh, Maritim Golf hotel yestarday evening,President Kikwete is in Egypt for the 4th ministerial conference on China- Africa Cooperation(photo by Freddy Maro)

Sunday, November 8, 2009

MAISHA CLUB ILIVYOTEKETEA KWA MOTO LEO MCHANA!!

Kama linavyoonekana jengo ilimokuwemo Maisha Club lilkiwa limeungua na kuteketea kabisa kutokana na moto ambao unadaiwa kuanza kuwaka mida ya saa saba mchana hata hivyo imeelezwa kuwa vikosi vya kuzima moto vilichelewa kufika katikaeneo la tukio na kukuta moto huo umesambaa eneo kubwa na kuunguza sehemu kubwa ya club hiyo na kuunguza karibu vifaa vingi vilivyokuwa vikitumika katika club hiyo hali ndiyo kama hivyo wadau tunampa piole mama yetu Hellen Swea na msimamizi wake Dj Majay kwa kupatwa na matatizo hayo mungu awape nguvu na ujasiri katika kipindi hiki kigumu kwako.
Vyombo vya muziki vikiokolewa kutoka katika club hiyo na wafanyakazi wa vikosi vya kuzima moto hata hivyo moto huo umeteketeza mali nyingi ambazo mpaka sasa thamani yake bado haijafahamika.

Wafanyakazi wa kikosi cha kuzima moto wakijaribu kuzima moto huo bila mafanikio kwani karibu jengo zima la club hiyo limeungua.

Moto ukiteketeza majengo a club hiyo ya usiku leo mchana vifaa vingi vimungua kwa moto na kuteketea.




Shilingi 112,080,000 zinatarajiwa kutumika kujenga zahanati ya Lusoga iliyopo wilayani mbinga!!

Mama Salma Kikwete akiwa amemshika mtoto.
Na Anna Nkinda - Maelezo, aliyekuwa Ruvuma
08/11/2009 Jumla ya Tshs. 112,080,000/= zinatarajiwa kutumika kwenye ujenzi wa zahanati ya Lusoga iliyopo wilayani Mbinga katika mkoa wa Ruvuma.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa wakati akikabidhi ripoti ya wilaya ya Mbinga kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa wa Ruvuma.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwezi wa tisa mwaka huu hadi sasa wananchi wameshiriki kuleta matofali ya kuchoma 70,000, mawe tripu 60 na uchotaji wa maji kwa ajili shughuli za ujenzi hivyo kufanya nguvu za wananchi kufikia Tshs. 5,800,000/=.
"Halmashauri kwa upande wake inakusudia kugharamia uwekaji wa umeme, maji pamoja na uzio wa zahanati kazi itakayogharimu Tshs. 30,000,000/= pia wahisani kutoka Jamhuri ya watu wa Korea kupitia shirika la Medical Peace Foundation wametoa mchango wa Tshs. 82,080,000/= na hadi sasa wametoa kiasi cha Tshs. 24,730,413.02", alisema Kanali Mstaafu Mjengwa
Aliendelea kusema kuwa lengo kuu la ujenzi wa zahanati hiyo ni kupunguza msongamano katika Hospitali ya wilaya kwa kuweza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi kwani ujenzi wa zahanati hiyo ukikamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 7,000.

Saturday, November 7, 2009

MZEE ALEX MUKAMA KUSAGA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI!!

Mtoto wa marehemu mzee Alex kusaga na Mkurugenzi wa Radio Clouds Joseph Kusaga na mke wake Juhayna pamoja na mtoto wao wa kwanza Natalia wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mzazi wa mpendwa,Mzee Alex Kusaga alifariki hivi karibuni nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Kansa.
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba akiweka shada la maua katika kaburi.
Mwenyekiti mtendaji wa Makampuni ya IPP na mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) Bw. Reginard Mengi akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mzee Kusaga kwa niaba ya vyombo vya habari.
Hii ni moja ya Camera maalum zilizokuwa zikirekodi na kurusha tukio hilo moja kwa moja kwa watu waliokuwa wamehudhuria mazishi hayo kupitia luninga kubwa iliyokuwa imewekwa makaburini hapo.
Jeneza la marehemu Mzee Kusaga likiwa limewekwa tayari kwa kushushwa kaburini.
Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akiongoza msafara kuelekea mahali pa kuhidhi mwili wa marehemu Mzee Alex Kusaga mara baada ya ibada fupi ya mazishi makaburini hapo.
Wanafamilia wa Marehenu mzee Alex Kusaga wakiwa wamekaa kwa masikitiko.

Wasanii wa kikunsdi cha THT wakiimba nyimbo za maombolezo kwenye mazishi ya mzee Alex Kusaga.
Watangazaji wa Radio Clouds wakiomboleza msiba wa bosi wao.

Wafanyakazi na ndugu jamaa na marafiki wa Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Clouds Entarteinment wakifuatilia kwa karibu wakati wa ibada ya mazishi katika makaburi ya Kinondoni leo.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana na lihimidiwe AMIN

WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA KISASA HOSPITAL YA MKOA WA DODOMA!!

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wa pili kutoka kushoto akikata utepe pamoja na makamo wa rais wa Abbott Fund Tanzania Christy Wistar kuzindua Maabara ya kisasa iliyojengwa katika Hospital kuu ya mkoa wa Dodoma na Mfuko wa Abbott Fund kushoto kwa waziri mkuu,wakishuhudia kushoto Naibu waziri wa Afya Dr Aisha Kigoda,Dr John Vertefeuille(kulia)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda watatu toka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Abbott Fund Tanzania,mara baada ya kuzindua rasmi maabara ya kisasa iliyojengwa na Abbott Fund katika Hospital kuu ya Mkoa wa Dodoma.

Bendera ya Taifa yafika kileleni Kilimanjaro!!

Elly Gerald Minja
BENDERA ya Taifa iliyokimbizwa kwa miguu na wanariadha nyota kwa sikutano mfululizo, hatimaye jana ilifika kileleni mwa mlima mrefu kulikoyote barani Afrika, Mlima Kilimanjaro na kusimikwa rasmi kwenye kilelecha Uhuru kilichopo umbali wa futi 5895 kutoka usawa wa bahari.Mwanamichezo mwenye uzoefu wa aina yake katika kuupanda mlima huo,Elly Gerald Minja ndiye aliyeifikisha bendera hiyo mapema janaasubuhi.
Mbali ya Minja mkazi wa mkoani Kilimanjaro, wanariadha mashujaawalioandika historia ya kuzindua mbio hizo za aina yake nchiniwalikimbiza bendera huku wakipokezana kila baada ya kilomita kati ya10 na 15 kutoka Dar es Salaam hadi Marangu, Moshi mkoani Kilimanjarotangu Jumapili iliyopita.Zaidi ya wanariadha 70 nchini, wengi wakiwa wa kimataifa walikimbizabendera hiyo kwa zaidi ya kilomita 567. Walifika Marangu Alhamisijioni na siku iliyofuata baadhi yao walianza kuipandisha MlimaKilimanjaro bendera hiyo ambayo mbio zake zimeasisiwa na kudhaminiwana Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.
Nyota kama Francis Naali na binti yake, Mary Naali aliyeipa Tanzaniamedali ya shaba katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Beijing,China, Samwel Mwera, Sarah Maja walikuwa kivutio kikubwa kamailivyokuwa kwa Peter Pallagyo, mkongwe mwenye umri wa miaka 50 namalemavu wa mikono aliyewaikilisha nchi katika michuano ya Olimpiki naJumuiya ya Madola, Joro Mathias.Akiwa mwenye furaha isiyo kifani mara baada ya wanariadha kufikaMarangu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisemaamefurahishwa na jinsi Watanzania walivyozipokea mbio hizo za ainayake nchini.“Ninawashukuru ndugu zangu Watanzania kwa sababu bila ya ninyi kamwetusingefika hapa, asanteni kwa kuwaunga mkono wanariadha waliokimbiakwa umbali mrefu kutoka Dar es Salaam hadi hapa, na asanteni kwakuiunga mkono Bia ya Kilimanjaro…tunaahidi kuendelea kuwafanya makubwazaidi Watanzania…“Tunajivunia mlima mrefu kuliko yote Afrika na tunajivunia bia yetu yaKilimanjaro…hatuna budi kuungana kuvitangaza vivutio vyetu,”alisisitiza Kavishe huku akielezea umuhimu wa mbio hizo zilizopewajina la “Fikisha Tanzania Katika Hatua za Juu”.

KILIMANJARO MARATHON 2010 YAZINDULIWA!!

Afisa Uhusiano wa kampuni ya Bia nchini TBL akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2010 uliofanyika jana kwenye Hoteli ya New Africa kulia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Executive Solutions Bw. Alan Turner, mbio Kilimanjaro Marathon hushirikisha wanariadha walio maarufu na wasioa maarufu kutoka mataifa mbalimbali hivyo kuongeza utalii nchini na kuvumbua vipaji vya wanariadha nchini mwetu.
Wasanii wa kundi la THT wakifanya vitu vyao wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2010 uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa baraza la Michezo BMT Kanali Idd Kipingu akizindua rasmi mbio za Kilimanjaro Marathon 2010 zinazofanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro, uzinduzi huo ulifanyika jana kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es ,wanaoshuhudia tukio hilo kulia na Emilian Rwejuna meneja udhamini wa Vodacom Tanzania na Dorris Malulu Afisa Uhusian TBL.

Mwenyekiti wa baraza la michezo nchini Kanali Idd Kipingu wa tano kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa Kilimanjaro Marathon na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo mara baada ya uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon 2010 kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam jana.

Wenger unconcerned by goals against!!

Arsene Wenger
Arsene Wenger has no doubts Arsenal's defence will soon be among the meanest in the Barclays Premier League once again. The Gunners head to Wolverhampton Wanderers for today's late afternoon kick-off on the back of some fine form, looking to extend an unbeaten run of 12 matches in all competitions.
However, while Arsenal may be the leading scorers in the top flight with 32 goals from the opening ten matches, they have also conceded 13, more than any other of the top four. Wenger, though, does not feel overly concerned.
"We can score goals and open teams up, which is a good basis to have confidence," he said. "It also makes you keen to work on the defensive side of your game. That is a concern, but I do not think it is a problem.
I am happy with our team-work defensively and confident our defensive record will improve.
Arsenal manager Arsene Wenger
"When you analyse the numbers a bit deeper, we conceded goals in high-scoring games where our attention eased off a bit. Also, we have had something like only 36 shots against us, which means defensively we are quite sure," said Wenger. "I am happy with our team-work defensively and confident our defensive record will improve."
Despite leaking the odd goal or two, Arsenal's new central defensive partnership of Thomas Vermaelen and veteran William Gallas has impressed. Belgian international Vermaelen, a £10m summer signing from Ajax, has slotted straight into the heart of the backline, in the wake of Kolo Toure's move to Manchester City.
With Johan Djourou unavailable until spring as he recovers from knee surgery, Philippe Senderos and Mikael Silvestre provide the back-up for what is set to be a hectic return to action following the international break.
Wenger, though, insisted: "At the moment, I am not tempted to rotate [my centre backs]. I do not like to rotate too much in central defence because we are in a position where they have a good understanding and every point is vital, so it is not worth to take a gamble if I am not forced to do it."
The Arsenal manager added: "Senderos is coming back into a good condition, Silvestre is working very hard and looking very good in training, so we are covered, but of course, you want to keep everybody in match fitness."
Vermaelen paid tribute to the way his defensive team-mates helped him settle quickly at Emirates Stadium.
"William is playing very well this year and it makes it easier for me to play in this team," said the Belgian. "It is important to have these good players because it makes it easier to fit in." story by www.fifa.com

RAIS JAKAYA AKITOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU NG'ITU!!

Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ruangwa Sigfrid Ng"itu kijijini kwake Mibule Ruangwa kabla ya mazishi kufanyika 6.11.2009.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbuge wa Ruangwa Sigfrid Ng'itu kijijini kwake Mibule Ruangwa jana mchana


Friday, November 6, 2009

Big Brother Revolution: Images from Day 60 - THURSDAY NOVEMBER 5

Day 60 on M-Net’s Big Brother Revolution and after completing their new garden the housemates prepare for their task presentation. Big Brother has instructed them to host a summer-themed cocktail party which includes a tour of the new garden explaining the concept, design and layout. Meanwhile on completion of a successful presentation the housemates celebrate as Big Brother informs them that they have won their Green Revolution task. Tune in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199 and for more information, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.

MWENYEKITI WA IPP AKIONYESHA KADI YAKE YA CCM!!

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Bw Rerginand Mengi akionyesha kadi yake ya unachama wa chama cha mapinduzi mbele ya waandishi wa habari wa vyombo mblaimbali wakati alipoongea nao ofisini kwake jengo la Hidary Plazza jijini Dar es salaam leo, Mengi amesema kadi hiyo aliikata mwaka 1977 na kuwa mwanachama halali wa chama hicho.

KOMBE LA LIGI KUU UINGEREZA KUONYESHWA KWA MASHABIKI JIJINI DAR!!

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays nchini Bw. Rashed Bade kulia na mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT Kanali Idd Kipingu wakifunua kitambaa ili kuonyesha kombe la Ligi kuu ya Uingereza (English Barcklays Premier Ligue Cup) mbele ya waandishi wa habari kwenye Hoteli ya New Africa jijini leo, kombe hilo litakimbizwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa siku mbili mfurulizo ili kuwapa fursa mashabiki mbalimbali wa timu za Uingereza waliopo nchini kuliona. ,

RATIBA YA MAZISHI YA MZEE ALEX KUSAGA!!

Ratiba ya Mazishi ya Marehemu Mzee Alex Kusaga Novemba 7 -2009 kama inavysomeka hapa chini katika jeduari.

RAIS KARUME, SEIF SHARIF HAMAD WAKUTANA IKULU ZANZIBAR!!

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Rais wa Zanzibara na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Aman Abeid Karume leo wakati alipomtembelea rais huyo katika ikulu ya Zanzibar, Kulia ni Mkurugenzi wa mambo ya nje wa CUF Ismail Jussa hii ni mara ya kwanza kwa Seif sharif Hamad kumtembelea Rais Karume kwa mazungumzo na haijajulikana walizungumzia nini (Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu Zanzibar).

Catch all the 2009 Channel O Music Video Awards action!


This year’s Channel O Music Video Awards have been applauded as the best ever – and viewers can now be part of the action when Africa’s leading awards event is broadcast on Sunday 8 November.
Carnival City was the venue for the event, which saw Africa’s top artists turn out to celebrate the best and most brilliant that the continent has to offer. And what a line-up of stars it was!
The red carpet was abuzz with action as the nominees, performers and celebrities made their way into the Big Top Arena on the evening of October 29th. From South Africa’s own Da L.E.S to Zimbabwe’s Buffalo Souljah, Namibia’s Gal Level and Nigeria’s Darey Art Alade, the style and sass of Africa’s biggest stars can be seen on Sunday night’s broadcast when the Channel O Music Video Awards Red Carpet Special kicks off at 20:30 CAT.
Come 21:00 CAT it’s time for the real fireworks to begin as a parade of winners take to the podium to receive their awards, much to the delight of their fans in attendance. The real highlight of this year’s Channel O Music Video Awards were the live performances, which included a tribute to Special Recognition award recipient, Brenda Fassie. In what many concluded was the heart and soul of this year’s event, Brenda’s son, Bongani (of Jozi fame) and Winnie Khumalo ignited the stage with renditions of two of Brenda’s biggest hits – ‘Weekend Special’ and ‘Vulindlela’.
Other performances came from Nigerian singer-songwriter, Nneka, South Africa’s own HHP, African Hip-Hop Royalty for the Emcee Africa II winner track “All Around Africa” as well as TKZEE in one of their first live television performances since getting back in the studio.
The show closed in roaring style with a sizzling hot performance by Mozambique’s Lizha James who brought down the house with her Afro centric number. Also adding to the night’s super-charged entertainment were hosts Vuzu presenter Nonhle and Channel O’s own Lungile and KB. They were joined by an impressive lineup of guest presenters including Channel O VJs Chuma, the Twinz, Enhle and Top Mais host, Weza.
So don’t miss out on seeing Africa’s best and biggest stars in full flight! Tune in to the 2009 Channel O Music Video Awards on Sunday 8 November at 20:30 CAT for the Red Carpet Special and 21:00 CAT for the awards event itself.

With hunger rising, food emerges as key to security, poverty and climate!!

UN General Secretary Ban Ki Moon.

An upward spike in the number of hungry people worldwide, and a realization that long-term challenges lie ahead in feeding the planet’s growing population, are pushing food security into the centre of global policy concerns for the first time in decades. What’s more, policy-makers are finding that food security solutions are directly tied to other key objectives.
Under pressure from dwindling purchasing power since last year’s economic crash, the number of malnourished people in the world has now surpassed a staggering one billion. Food prices – although down globally from mid-2008 levels – continue to remain high in many of the poorest countries, as drought and floods take a toll on livestock and farmlands. Spurred by UN Secretary-General Ban Ki-moon’s High-Level Task Force on the Global Food Security Crisis, donors pledged $20 billion at the G-8 meeting in L’Aquila, Italy, in June this year, where 26 developed and developing nations endorsed a hard-hitting action plan. The “L’Aquila principles” notably place agricultural productivity and support for poor farmers on a par with emergency food aid, usually the more dramatic and better-bankrolled activity. Emergency aid, nevertheless, is now severely under-funded in relation to the impact of economic and weather-related shocks. The World Food Programme is urgently seeking to regain its level of 2008 support, when it led an $8 billion emergency mobilization against hunger, the largest in history.
Philanthropist Bill Gates has announced that his multi-billion dollar foundation will now focus mainly on food security. Making poor farmers more productive, he said, will have a massive impact on tackling world hunger. From 16-18 November 2009, the Food and Agriculture Organization (FAO) will hold a summit on food security, following up on its June 2008 emergency meeting. The Rome summit, says FAO Director-General Jacques Diouf, aims to “forge a broad consensus on eradication of hunger in the world.” Secretary-General Ban, who will attend, last week assigned inter-agency task force coordinator David Nabarro to also serve as his Special Representative for Food Security and Nutrition.

Thursday, November 5, 2009

VODACOM MISS TANZANIA MIRIAM GERALD AKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA!!

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi bendera ya Taifa Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald, mrembo huyo anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika tarehe 12 mwezi Disemba mwaka huu katika mji wa Sanddown nchini Afrika Kusini na ataondoka leo kuelekea nchini Uingreza ili kujiunga katika kambi ya Miss World pamoja na warembo wengine wanaowakilisha nchi zao.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bw. Emmanuel Ole Naiko akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald iliyofanyika kwenye ofisi za kituo hicho jijini Dar es salaam leo .



MAONYESHO YA SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA KWA MAFANIKIO!!

Mwadaaji wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali akiwa katika picha ya pamoja na mwandaaji wa Lady in Red. Asia Idarous wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya Swahili Fashion Week yaliyoanza jana na yanatarajiwa kuendelea mpaka Novemba 6 Jumamosi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo wabunifu wa mitindo mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wanaonyesha ubunifu wa nguo zao.
Onyesho hilo la jana lilionyesha ukomavu wa wabunifu wetu kutokana na ubora wa mavazi waliyoonyesha na viwango vya ubora wa onyesho lenyewe, ambapo wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali walihudhuria na kuonyesha kufurahishwa na maandalizi ya kazi za wabunifu walioonyesha mavazi yao na jinsi onyesho lilivyoendesha kwa ujumla.




Hapa wanamitindo wakaanza.
Wadau mbalimbali wakifuatilia Uzinduzi wa Maonyesho hayo ya Swahili Fashion Week Kutoka kushoto ni Kevin Twisa Mkurugenzi wa Masoko Zain Teweli Teweli Meneja Uhusiano wa Barrick na Mwanahabari Siddy Mgumia kutoka New Habari 2006.
Mdau Anitah Rex kulia kutoka Canada na rafiki yake Bupe wakipozi kwa picha.

Katikati Khadija Mwanamboka mbunifu ambaye pia alipata nafasi ya kuonyesha nguo zake.

Kutoka kushoto mdau Belinda , Sauda Simba na Happiness Mchaki
.
Kutoka kushoto ni Mwamvita Makamba mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Waziri wa Afrika Mashariki Amason Jeffa Kingi kutoka Kenya, Sofia Byanaku na mmoja wa waalikwa wakifuatilia kwa karibu onyesho hilo la mavazi wakati lilipozinduliwa jana kwenye viwanja vya Karimjee Hall.

Mwaandaaji wa maonyesho hayo ya mavazi ya Swahili Fashion Show Mustafa Hassanalia aliyekaa katikati akifurahia maonyesho hayo na waalikwa mbalimbali..
Wabunifu wa mavazi Asia Idarous na Ally Rehmtullah wakipiga makifi kuashiria kufurahishwa na onyesho hilo.

WATOTO 246,927 KUPEWA VYANDARUA VYENYE DAWA VYA KUJIKINGA NA MARALIA MKOANI RUVUMA!!

Mama Salma Kikwete na watoto.
Na Anna Nkinda - Maelezo, Ruvuma
05/11/2009 Jumla ya watoto 246,927 walio chini ya umri wa miaka mitano wanatarajiwa kupewa bure vyandarua vyenye dawa ili kuweza kupunguza tatizo la kuugua pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa maralia katika mkoa wa Ruvuma.
Hayo yamesemwa jana na mganga mkuu wa mkoa huo Dk. Daniel Malekela wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kugawa vyandarua bila malipo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ulifanywa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.
Dk. Malekela alisema kuwa walifanya sensa ya kutambua idadi ya watoto wanaostahili kupata vyandarua hivyo na jumla ya vyandarua 274,687 vimeshasambazwa katika vijiji na mitaa 539 ya mkoa huo hii inamaana kuwa kuna ziada ya vyandarua 27,760 ili na wale watoto waliozaliwa baada ya sensa kupita wapate
Licha ya kugawa vyandarua vyenye dawa mkoa huo pia unatarajia kuviwekea dawa vyandarua vipatavyo 254,400 vinavyotumika katika kaya bila jamii kuchangia gharama zozote zile.
"Tumeamua kufanya kampeni hii kwani katika tafiti ya kitaifa iliyofanywa mwaka 2007/2008 inaonyesha kuwa ni kaya nne tu kati ya 10 zinatumia chandarua kimoja chenye dawa hii inaonyesha kuwa kaya nyingi katika jamii yetu hazitumii vyandarua vyenye dawa na hivyo kuwa katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa malaria", alisema Dk. Malekela.
Aliendelea kusema kuwa takwimu za mwaka 2008 zinaonyesha kuwa asilimia 55 ya wagonjwa wote waliopata huduma katika vituo vya kutolea huduma wenye umri chini ya miaka mitano waliugua ugonjwa wa maralia na vifo chini ya miaka mitano vilikuwa ni asilimia 56 ya vifo vyote vilivyotolewa taarifa.
Akizindua kampeni hiyo Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa lengo la Serikali kutoa vyandarua hivi ni kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa maralia na si vinginevyo kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuviuza na wengine hata kuvivulia samaki haya ni matumizi mabaya ya vyandarua hivi.
Mama Kikwete alisema kuwa kila mtoto anayo haki ya kulala ndani ya chandarua kilichowekwa dawa ya kuua mbu waenezao ugonjwa wa maralia ili kupunguza kiwango cha vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.
"Ninawaomba na ninawasisitizia wazazi wote kuwa ni muhimu kumuwahisha mtoto Hospitali pindi anapoonyesha dalili za kuugua ugonjwa wa maralia ndani ya masaa 24 hii inaweza kuokoa maisha yake kwani kumchelewesha ni hatari sana pia baadhi yenu muache tabia ya kuwapeleka watoto wenu kwa waganga wa kienyeji kwani utakuta mtoto anadalili zote za maralia lakini mzazi anampekea kwa waganga wa kienyeji jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kupelekea kifo cha mtoto wako", alisema.
Ugonjwa wa maralia unashika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Ruvuma kwani kuna idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa kiwango cha asilimia 23.9 pia takwimu za mwaka 2004 - 2008 zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa maralia mwaka hadi mwaka. Katika kipindi hiki asilimia 50.3 ya wagonjwa wote wa maralia walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka mitano na zaidi ya miaka mitano walikuwa ni asilimia 49.7.
Wakati huohuo Taasisi ya WAMA iliwapatia kituo cha afya Madaba msaada wa vitanda vya kujifungulia viwili, Delivery kit moja, vitanda vya Hospitali vitano, magodoro matano, mashuka kumi,Stethosope moja, mzani wa kupimia uzito wa watoto moja, mzani wa kupimia uzito wa watu wazima mmoja na trolley dressing moja. Thamani ya vifaa vyote hivi ni Tshs.4,483,000/=.

Big Brother Revolution: Images from Day 58 - TUESDAY NOVEMBER 3!!


Day 58 on M-Net’s Big Brother Revolution and the housemates welcome a new addition to the house, as “man’s best friend” Ruby makes her appearance. Meanwhile the housemates have been given the formidable task of creating a new garden for the Big Brother house and have been busy planting, watering and digging! And the tension grows as the days pass and another eviction looms ever closer! Tune in to Big Brother Revolution on DStv channel 198 or 199 and for more information, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.

Wednesday, November 4, 2009

Bia ya Kilimanjaro yamzindua DC Same!!

Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahimu Marwa (kushoto) akimkabidhi bendera ya taifa mwanariaadha, Francis Naali kabla ya kuanza kwa mbio maalumu za kukimbia mbio maalum za kukimbiza bendera ya taifa hadi kilele cha mlima kilimanjaro.Mbio zenye ujumbe wa “Fikisha Tanzani katika hatua ya juu zaidi” na kudhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro.

Mwanariadhaa, Francis Naali akianza mbio maalum za kukimbiza bendera ya taifa hadi katika kilele cha mlima kilimanjaro. Mbio hizo zilianza jana wilayani same huku zikiwa na ujumbewa "Fikisha Tanzania katika hatua ya juu zaidi" zimedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro.

Na Mwandishi Wetu, Same

MAPOKEZI makubwa ya wanariadha wanaokimbiza bendera ya Taifa kwenda kilele cha Mlima Kilimanjaro, yamemzindua Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahim Marwa na sasa ameahidi kuelekeza nguvu zake katika kukuza mchezo huo wilayani mwake.
Marwa aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa anakabidhi bendera ya Taifa kwa mwanariadha nyota Francis Naali, aliyeanzisha ngwe ya mwisho ya mbio hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.
Naali alikuwa anaanzisha mbio kumalizia kilomita 104 kati ya 567 walizokimbia wanariadha zaidi ya 70 tangu kuanza kwa mbio hizo Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam na kuendelea kwa siku nne mfululizo, zikipita katika mikoa ya Pwani, Tanga na hatimaye Kilimanjaro.
“Jamani, nimehamasika sana na ninawashukuru Bia ya Kilimanjaro kwa kuipa Same heshima ya kuwa na kituo cha mbio hizi. Binafsi nimehamasika na ninatangaza rasmi kwamba, kuanzia sasa nitaweka mkazo katika riadha wilayani kwangu.
wakiianza ngwe ya mwisho ya mbio hizo.
Naye Meneja Masoko wa TBL, David Minja akiwa mwenye tabasamu, alisema: “Tunajivunia kampeni hii ya kupandisha bendera katika Mlima Kilimanjaro, na kikubwa tunashukuru kwa jinsi Watanzania walivyopokea kampeni hii ya “Fikisha Tanzania Katika Hatua za Juu”. Tunajivunia mlima mrefu kuliko yote Afrika na tunajivunia bia yetu ya Kilimanjaro…”
Kauli ya shukrani kwa wakazi wa mikoa waliyopitia wanariadha hao ilitolewa pia na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Alisema; “Leo ni siku ya nne ya mbio hizi za aina yake na tunashukuru kwa mwamko ambao Watanzania wameuonyesha kote tulikopita.Sisi wa Bia ya Kilimanjaro tuko kamili na tunajipanga kuhakikisha mbio hizi zinapata mafanikio zaidi na zaidi, lengo likiwa kwenda sambamba na umaarufu wa mlima wa Kilimanjaro.”
Bia hiyo, ndiyo inayozidhamini klabu kongwe na maarufu zaidi katika soka nchini, Simba na Yanga, pia ni mdhamini wa muda mrefu wa mbio za kimataifa za Marathoni za Kilimanjaro na zile zinazoshirikisha wanariadha kutoka zaidi ya nchi 25 duniani.
Pia ni wadhamini wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro. Imekuwa pia ikidhamini michuano ya mpira wa kikapu ya mkoani Dar es Salaam `RBA Kili’.
Mbio hizo zilitarajiwa kuingia Marangu jana jioni, tayari kwa kuipandisha kileleni mwa Mlima Kilimanjaro, leo.

IDADI YA WATEMBELEAJI